ZURICH, USWISI
Anthony Martial (katikati) akifunga bao dhidi ya Liverpool, Clyne (kushoto) akisindika kwa macho |
KUNA washambuliaji wengi katika
ulimwengu wa kandanda katika Ligi Kuu nchini Tanzania utakutana na namba tisa
wengi kama John Bocco, Amis Tambwe, Donald Ngoma, Malimi Busungu na wengine
wengi.
Nje ya Tanzania utawaona
Michael Olunga (Kenya), Edin Dzeko (Bosni-Herzegovina), Luis Suarez (Uruguay),
Clint Dempsey (Marekani), Mario Balotelli (Italia) na kadhalika.
Mfano wetu utaanzia kwa nyota
aliyekuwapo Liverpool ya England na sasa yupo katika klabu ya AC Milan huyo ni
Mario Balotelli.
Alipokuwa Liverpool wengi
walikaririwa wakisema uwezo wa nyota huyo umekwisha hivyo kocha wake wakati huo
Brendan Rodgers ikaonekana alifanya usajili usio kuwa na macho akimwacha
Luis Suarez atimkie Barcelona ya Hispania.
Swali ni kweli Balotelli alikuwa
akichezeshwa kama yeye alivyo au kocha Brendan alikuwa akimtengeneza kwa ajili
ya nafasi nyingine, jibu kale tutalipata mbele.
LEO tujikite katika uchambuzi wa
namba washambuliaji wanavyotakiwa kuwa ili kuzifanya timu kuwa na matokeo
mazuri dimbani.
Mshambuliaji wa shabaha
Nguvu, uimara na umbo linaloonekana
ni mahitaji ya kwanza kwa ‘foward’ yeyote duniani.
Uwezo wa kukaa na mpira na uwezo wa
kuuweka mwili wake kati ya mlinzi wa timu pinzani na mpira ni sifa muhimu
katika nafasi ya ushambuliaji.
Anapaswa kuwa na uwezo wa kukaa na
mpira ili awaruhusu wachezaji wenzake kufika na kutengeneza mashambulizi.
Timu nyingi hupenda kuwatumia
washambuliaji wa jinsi hii ili kupata matokeo mazuri.
Kwa mfano Chelsea, Stoke City, West
Ham katika Ligi Kuu ya England (EPL) na Real Madrid katika La Liga.
Jamie Carragher wa Liverpool aliwahi
kumsifia Rick Lamert kuwa ni mshambuliaji mwenye shabaha kuliko Balotelli, je
ni kweli?
Mshambuliaji mwenye shabaha ni lazima
awe na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti yenye nguvu yanayolenga goli ili kuwachanganya
walinzi wa timu pinzani.
Hapa utakutana na nyota kama Peter
Crouch, Wilfred Bony, Diego Costa, Riobin van Persie, Mario Mandzukic, Didier
Drogba na wengine.
Washambuliaji hawa wamebarikiwa sana
huwa ni wazima sana wanapopata mipira ya hewani pia hutoa msaada mkubwa wakati
wa kulinda kona zinapopigwa kwenye lango lao na mapigo huru.
Mshambuliaji mwizi
Unawakumbuka Ruud van Nistelrooy,
Filipo Inzaghi na Raúl Gonzalez walipokuwa katika ubora wao?
Washambuliaji hawa siku zote
hawakusimama pekee yao wakisubiri kuletewa mipira kama barua lakini walikuwa na
kipaji cha kujua ni wapi wasimame ambako ni sahihi kwa muda
mwafaka.
Uwezo wao mkubwa wa umaliziaji
katika eneo lolote ndani ya kisanduku cha penalti uliwafanya wang’are
isivyokuwa kawaida.
Utamjua tu pindi atakapoukwamisha
mpira katika nyavu za lango la mpinzani lakini unaweza kujiuliza mbinu
aliyoitumia.
Jibu lake ni jepesi tu,
walikuwa makini na haraka kuiba mipira kwa wachezaji wa timu pinzani pindi
wanapozubaa katika kisanduku cha penalti.
Hapa kuna mchezaji mahiri kutoka
Cameroon, Samuel Eto’o hakika utamkubali nyota huyo kwa wizi aliokuwa akiufanya
katika kisanduku cha goli la mpinzani na kuukwamisha mpira wavuni.
Sir Alex Ferguson aliwahi kusema
kuhusu Inzaghi kuwa “Huyu alizaliwa kwa offside” akiwa na maana namna
alivyokuwa akijiweka katika uwanja utafikiri yupo ‘offside’ kumbe sekunde mbili
mbele yupo eneo jingine ukifunguka sekunde ya tano tayari ashafunga.
Namba 9 wa uongo
Mchezaji mwenyewe anaweza
kujitengeneza anapokuwa dimbani kuwa namba 9 wa uongo kama alivyo Lionel Messi
na Cristiano Ronaldo ambapo wao kwa asili sio ‘forward’.
Kwa kufanya hivyo utawachanganya
walinzi wa timu pinzani kwani utakuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira
na kutembea na mpira hatimaye utaweza kutoa pasi ya mauaji kwa ajili ya
kuangalia namna mtakavyocheza ‘One-Two’
Mfumo huo pia uliweza kumuibua Cesc
Fabregas kama ‘Namba tisa wa uongo’.
Jambo la msingi hapo ni kuwa mmwepesi
hali itakayokufanya uogopeke na walinzi wa timu pinzani.
Trequartista
Trequartista imekuwa maarufu sana
nchini Italia ambapo robo tatu ya uwanja hujazwa na forward au kiungo
mshambuliaji ambaye ataimiliki robo tatu ta uwanja huo .
Ataweza hivyo tu endapo ana uwezo
mkubwa kuwa kupiga pasi, kuona, kumiliki mpira na maarifa mengine ya kandanda
lakini kubwa zaidi ni uwezo mzuri wa kupiga katika lango la mpinzani.
Utawakumbuka Diego Maradona, Zinedine
Zidane, Riquelme na Johan Cruyff, Alessandro del Piero.
Kwa sasa utakutana na David Silva,
Isco na Juna Mata pia Rooney.
Mshambuliaji anayepanua uwanja
Hapa huwezi kumuacha Cristiano
Ronaldo, Gareth Bale na Alexis Sanchez.
Mara nyingi mshambuliaji wa
aina hii hupenda sana kucheza katika winga huku wakijivunia kuwa na mguu
imara, kasi na stamina.
Timu zinazopenda kutumia mashambulizi
ya ghafla basi huwatumia sana nyota wa jinsi hii ambao wana nguvu za kuwazidi
walinzi wa pembeni (full backs).
Comments