SIO
wachezaji wote hupata bahati ya kushiriki michuano ya olimpiki katika maisha
yao hususani katika mchezo wa kandanda.
Hata hao waliobahatika huweza kutwaa medali mbili tu.
Hata hao waliobahatika huweza kutwaa medali mbili tu.
Miongoni
mwao ni Muargentina Roberto Fabian Ayala ambaye alifanikiwa kuitumikia timu ya
taifa katika michuano iliyofanyika Atlanta, Canada mwaka 1996 na ile ya mwaka
2004 jijini Athens nchini Ugiriki.
Alipewa
jina la ‘El Ratón’ na mashabiki yaani
‘The Mouse’ kifaa kimojawapo katika kompyuta.
Nyota
huyo anasimulia namna ambavyo ina maana kwa mchezaji wa kandanda wa kiwango cha
Kimataifa anapoitumikia nchi yake katika michuano ya Olimpiki.
Kwa
miaka 15 Ayala alikuwa nyota na nembo ya La Albiceleste.
“Unapokuwa
mchezaji, ndoto zako na malengo ni kucheza Kombe la Dunia. Lakini michuano ya
Olimpiki ni tofauti kabisa unapotaka kucheza cha kwanza kabisa ni pale
unapostaajabishwa na wanamichezo wote kukaa katika kijiji kimoja.”
Ayala
ambaye amewahi kuhudumu River Plate, Napoli, AC Milan, Real Zaragoza katika
nafasi ya ulinzi wa kati anaongeza, “Nilikuja kujua katika olimpiki yangu ya
pili nini maana ya kuwa mwanamichezo. Atlanta ulikuwa mji wa tofauti na ulikuwa
mbali lakini mwaka 2004 tulipokaa katika kijiji cha olimpiki niliweza kujionea
roho za michezo ya ridhaa ilivyo katika eneo hilo. Muulize mchezaji yoyote
dunia mahali popote huwa kinatokea nini ukiwa hapo.”
Hatasahau
Mwaka
1996 Nigeria ilizabua Argentina mabao 3-2. “Tulipoteza katika dakika za mwisho,
wakati tukitaka kucheza mtego wa offside, tulikosolewa sana kwa aina hiyo ya
uchezaji. Tulijiandaa kwa kila hatua na ilikuwa sahihi kuitumia wakati huo,”
alisema Ayala na kuongeza.
“Tatizo
lilikuwa ni moja tu, mchezaji wetu mmoja alibaki. Tulithubutu kufanya hivyo na
ikatugharimu. Nigeria ilikuwa timu nzuri
sijawahi kuona. Hatukuweza kupoteza kwa timu ya zamani. Ilikuwa
ikitutesa sana kwa wakati huo, lakini tukaja kutambua kuwa medali na uzoefu
ndio vya thamani,” alisema nyota huyo.
Miaka
minane baadaye walitua jijini Athens, ambako Argentina ilitua na fasheni
iliyowafanya kutwaa medali ya dhahabu. Kwa kufanya hivyo walishinda michezo
sita wakitupia wavuni mabao 17 na kuruhusu moja huku wakimtambulisha rasmi
mshambuliaji Carlos Tevez ambaye alitunukiwa tuzo ya ‘Fair Play’.
“Tulipoteza
fainali ya Copa America, ilitutia uchungu sana. Timu ili haikuruhusu hata bao
moja ikicheza kandanda safi. Binafsi ninakumbuka nililia sana baada ya mchezo
ule, nilipiga magoti na kumkumbatia Javier Mascherano tulipotwaa medali pale
Athens, ilikuwa ni taji kubwa maisha kuwahi kushinda nikiwa na timu ya taifa,”
alisema Ayala.
Nyota
huyo wa Argentina mwenye miaka 43 ametoa hamasa kwa kikosi cha sasa cha taifa
lake kuwa kinapaswa kupambana kupata medali kwani kina kila sifa za kuweza
kufanya hivyo.
Ikumbukwe
kwamba ni mchezaji ambaye anashikilia rekodi ya kucheza mechi niyingi kuliko
mchezaji yeyote mechi 115 na 63 kati ya hizo akiwa ni nahodha wa La Albiceleste.
Comments