Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imesema uchakataji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura umekamilika na wamebaini kasoro ndogo ndogo takriban 300 ambazo zimeondolewa. Mkurugenzi wa Daftari na Tehama wa Nec, Dk. Modest Kipilimba, alisema walianza na kasoro 17 zilizobainishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Ukawa walibainisha kasoro hizo katika kituo cha mpigakura cha Ofisi ya Kitongoji Azimio 1, chenye namba 10101010102, kilichopo mtaa wa Mahoma/Makulu, Kata ya Chahwa, jimbo la Dodoma Mjini. Ukawa walibainisha vivuli, mabati, hoteli, watu waliojipiga picha wenyewe, Wazungu, Wachina na vivuli vikiwa vimepewa namba ya mpigakura na majina yasiyoeleweka. “Tumeondoa kasoro nyingi sana na kituo cha Azimio kwa sasa hakuna kasoro yoyote, mbali na kasoro hizo, kasoro nyingi ni za jinsia, kujirudia, jina kutokuonekana, ...