Skip to main content

Yanga yaisambaratisha Coasta


Send to a friend


Mshambuliaji wa Yanga, Davis Mwape akimtoka beki wa Coastal Union, Mbwana Hamis wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda mabao 5-0. Picha na Jackson Odoyo.

Sosthenes Nyoni

MSHAMBULIAJI Kenneth Asamoah alifunga mabao mawili na kuiongoza Yanga kuwasambaratisha vibonde wa ligi Coastal Union kwa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabingwa hao waliopoteza mvuto kwa mashabiki wao kutokana na kuanza ligi kwa kusuasua jana walionekana tofauti kabisa kwani katika dakika ya nne mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ghana, Asamoah alifunga bao la kwanza kabla ya Shamte Ally, Davies Mwape, Nurdin Bakari na Mghana huyo kufunga kalamu hiyo ya kishindo.

Kiungo Idrisa Rajabu alitoa mchango mkubwa kwenye mauaji hayo kwa kutengeneza mabao matatu kati ya matano ikiwa ni mechi yake ya tatu kuanza kuitumikia Yanga.

Umakini huo wa safu ya ushambuliaji ya Yanga unamfanya kocha Sam Timbe kutomfikiria kabisa mshambuliaji wake Jerryson Tegete aliyefunguliwa na uongozi wake hivi karibuni.

Timbe aliwapumzisha Mwape, Shamte na Asamoah na kuwaingiza Rashid Gumbo, Julius Mrope na Hamis Kiiza.

Mabingwa hao sasa wamefikisha pointi 12, huku Coastal wakibaki mkiani na pointi zao nne katika ligi hiyo inayoongozwa na Simba yenye pointi 18.

Mshambuliaji Davies Mwape alijaribu kufunga bao la mapema katika dakika ya 2, lakini mpira wake wa kichwa ulidakwa na kipa wa Coastal Union, Omar Hamis na dakika mbili baadaye Asamoah alifungia Yanga bao la kuongoza akimalizia kwa kichwa krosi nzuri ya Idrisa Rajabu.

Mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Kenya, Ben Mwalala alikaribia kuipatia timu yake bao katika dakika 11 baada ya kuunganisha vizuri krosi kutoka upande wa kulia iliyopigwa na Daniel Lianga, lakini kipa wa Yanga, Yaw Berko aliupangua mpira huo.

Winga Shamte Ally aliipatia Yanga bao la pili katika dakika ya 21 akiunganisha kwa umakini krosi ya Asamoah kutoka upande wa kushoto, wakati Wagosi hao wakishaanga uwanja wa Taifa, Mwape aliendeleza kalamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu kwa Yanga katika dakika ya 30 kwa kuunganisha kwa shuti kali pasi ya Rashid kutoka winga ya kushoto.

Mshambuliaji Mwalala alijaribu kuwaongoza vijana wake bila ya mafanikio kwa sababu katika dakika ya 35 alipiga shuti kali lililopanguliwa na Berko na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Nurdin Bakari aliipatia Yanga bao la nne katika dakika ya 41, akimalizia pasi nzuri ya Asamoah.

Yanga ambayo safu yake ya ushambuliaji ilikuwa ikilaumiwa kwa ubutu ilionekana kuwa bora mbele ya mabeki dhaifu wa Coastal Union ambao wameruhusu timu hiyo kufungwa mechi sita kati ya nane ilizocheza msimu huu.

Coastal mabingwa wa mwaka 1988 wanaofundishwa na Hafidh Bardu walishindwa kucheza kabisa na kumtegemea Mwalala wakati wapinzani wao Yanga wakitawala asilimia 80 ya ya mchezo huo katika nafasi ya kiungo na ushambuliaji.

Asamoah alipachika bao la tano katika dakika ya 46 akipokea krosi ya Rajabu na kuifanya Yanga kushinda kwa mabao 5-0. Asamoah amefunga mabao manne tangu msimu huu wa Ligi Kuu uanze.

Kocha wa Coastal Union, Badru alimpumzisha kipa wake Hamis aliyeruhusu mabao manne na kumwingiza Godson Mmasa, pia Coastal ilimtoa Mwinyi Abdulrahman na kumuingiza Said Swed.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was

HAYA NI MAKAO MAKUU YA MTANDAO WA Tigo TANZANIA DAR ES SALAAM

MAHALA yalipo ni Lugoda Street Gerezani Industrial Area , kwa sasa mdandao huu umefanya makubwa , kuna Tigo Bwerere Uilisha cheki hiyoooooo watu full kujiachia wana chonga tuu kwenye vyao vilonga.