Baadhi ya warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakipozi kwa picha katika kinyang’anyiro cha Vodacom miss talent 2011 ambapo Rose Albert alifanikiwa kunyakua taji hilo, hapo jana katika hotel ya Giraffe jijini Dar es Salaam.
Majaji wa shindano la Vodacom miss Talent 2011 wakiwa kazini,kutoka kushoto Jacqueline Walper,Rachel Sindbard,Bosco Majaliwa.
------
Na Mwandishi Wetu
Mrembo Rose Albert anaeshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, Jana aliwabwaga baadhi ya Washiriki wenzake aliochuana nao vikali na kunyakua taji hilo katika siku ya kuonyesha vipaji”Vodacom Miss Talent” iliyofanyika kwenye hotel ya Giraffe iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam.
Wakiadhimisha siku hiyo washiriki hao wa shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo nchini walichuana kwa kuonyesha vipaji vyao mbalimbali ikiwemo kuimba, kucheza miziki mbalimbali ya Bongo flava,nyimbo zetu za kiutamaduni,maigizo.
Akizungumzia siku hiyo Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao Matina Nkurlu alisema lengo la siku hiyo ni kutaka kutambua vipaji mbalimbali walivyonavyo warembo wakiwa tayari kuelekea kwenye hatua ya mwisho ya shindano hilo lenye hadhi ya kimataifa litakalofanyika mlimani city tarehe septemba 10.
Akifafanua Nkurlu alisema kwamba mbali ya kutaka kujua vipaji vyao pia imesaidia kuibua vipaji vya warembo hao mbali na fani ya urembo wanayojihusisha nayo.
“Tukiwa kwenye siku ya Vodacom Miss Talent warembo wameonesha vipaji vyao vya kipekee jambo lililowafanya pia kuendelea kuwa pamoja kama ilivyo tasnia hiyo kwamba inawaunganisha watu wote bila kujali dini rangi au kabila.
Nae mrembo Rose Albert alienyakua taji hilo amesema siku hiyo ni ya faida kwake kwani ameweza kuonyesha vipaji vyake mbalimbali alivyonavyo na kujifunza mengi toka kwa washiriki wenza .
Akifafanua Rose alisema mbali ya kuonesha viapaji vyake pia amepanua mtazamo wa kiakili kwani ni moja ya fani zinazoenda kushindaniwa katika shindano la Miss World kwa atakayebahatika kuliwakilisha Taifa letu.
“Vipaji ni moja ya vipengele kwenye shindano la urembo la dunia, hivyo kwa atakayebahatika atafanya vizuri kwani vipaji kitu muhimu tayari kwa kwenda kushiriki michuano hiyo ya urembo ya dunia.
Nae Mkuu wa kitengo cha Itifaki wa Kamati ya Vodacom Miss Tanzania Albert Makoye alisema ari waliyonayo warembo inaonesha utayari wao katika kuliwakilisha Taifa katika medani za kimataifa.
“Mmejionea wenyewe baadhi ya washiriki wetu walivyochuana katika shindano hili la Vodacom Miss Talent 2011 katika kuadhimisha siku ya vipaji kwa warembo. Hili tu linadhihirisha kwamba shindano la mwaka huu litakuwa na changamoto kubwa ikilinganishwa na mengine yaliyopita,” alisema Makoye.
Nawaomba watanzania wenzangu waendelee kuwapigia kura washiriki hao wanaoishi ndani ya jumba la Vodacom na watazame vituo vya televisheni Star tv na Clouds TV baada ya maisha yao ndani ya nyumba kuoneshwa moja kwa moja na vituo hivyo.
END.
Comments