Skip to main content

Lowassa apingwa kuchunguza Meremeta




Fidelis Butahe


BAADA ya Bunge kuikabidhi Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, jukumu la kuchunguza ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya Meremeta, wasomi na wanasiasa nchini wamepinga uamuzi huo wakidai kuwa ukweli utapindishwa.

Spika wa Bunge, Anne Makinda aliamua kuwa Kamati hiyo ya Bunge ifanye uchunguzi huo kwa kuwa ndiyo inayohusika na suala hilo la Meremeta.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili jana, wasomi na wanasiasa hao walidai kwamba, tatizo sio suala hilo kupelekwa katika kamati hiyo, bali ni mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye walisema hawaamini kama atafanya kazi hiyo vizuri.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Sengondo Mvungi alisema, “Inakuwaje mtu anatuhumiwa kwa mambo mbalimbali halafu kamati yake inapewa jukumu la kuchunguza suala hilo zito?”
Mvungi ambaye kitaaluma ni mwanasheria alisema kuwa, ni vyema kiongozi akiwa na tuhuma za kifisadi achunguzwe kwanza kabla ya kupewa majukumu.

“Hapa ndio utaona jinsi Serikali ya Tanzania inavyougua ugonjwa wa saratani ni lazima ife…, jambo hili katika taaluma ya sheria na katiba tunaliita kuwa ni ‘ishara ya dola inayokufa’,” alisema Mvungi.

Aliongeza: “Siku hizi si ajabu kuona jaji anahongwa na Takukuru… Ni wazi kuwa Serikali inayumba”.
Alisisitiza kwamba, ndani ya kamati hiyo atakayejiona hawezi kufanya kazi hiyo kwa kuwa ana maslahi binafsi na Meremeta aachie ngazi mapema ili kuondoa maswali kutoka kwa wananchi, kinyume chake uchunguzi wa kamati hiyo hautakuwa na faida yoyote.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alisema, “Jambo linaloibuliwa na kundi jingine na kuhitaji ufumbuzi si vyema likasimamiwa na kundi linalolalamikiwa”.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alisema kwa kiasi kikubwa sakata la Meremeta liliibuliwa na wabunge wa upinzani, lakini anashangaa kuona suala hilo linapi pelekwa katika kundi ambalo linaweza kuwa lilihusika.

“Simhukumu Lowassa kuwa ni fisadi…, lakini wakati Serikali inaingia mkataba na kampuni hii yeye alikuwa katika Baraza la Mawaziri, sasa suala hili kurejeshwa tena kwake ni sawa?” alihoji Mbowe.

Mbowe alisema kuwa huu ni wakati wa Bunge kutambua kuwa si lazima kila Kamati iongozwe na wabunge wa CCM na kusisitiza kuwa ni vyema ikaundwa Kamati itakayoongozwa na upinzani ili kuchunguza Meremeta.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema si lazima ufisadi wa Meremeta ukachunguzwa na Kamati ya Bunge.

“Takukuru si wapo wanaweza kufanya kazi hii…, hili ni jambo nyeti ambalo linatakiwa kuchunguzwa na watu wenye taaluma kama Takukuru, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Jeshi la Polisi,” alisema Mbatia.
Mbatia alidai kuwa ndani ya CCM hakuna wa kumfunga mwenzake kengele. Alidai kuwa chama hicho kimekithiri kwa ufisadi na kwamba walio salama ni wachache.

“Hakika uamuzi huu utazidi kuwachanganya Watanzania, inakuwaje mtu anatuhumiwa kwa mambo fulani halafu anachaguliwa kuwa Mwenyekiti Kamati ya Bunge, halafu kamati yake inapewa jukumu hili?” Alihoji Mbatia
Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, alidai kuwa kamati hiyo haiwezi kuja na majibu ya kuwaridhisha Watanzania.

“Ni usanii mtupu, hata vyombo vingine vya Serikali haviwezi kulichunguza jambo hili kwa kuwa kwa muda mrefu vimekuwa vibaraka wa mafisadi, labda vivunjwe na kuundwa upya,” alidai Mtikila

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana, alisema ingawa uamuzi huo wa Bunge utazua maswali mengi kwa wananchi, sheria za Tanzania zinaeleza wazi kuwa mtuhumiwa sio mkosaji.
“Mbona Lowassa anakwenda kanisani na kuchangisha mamilioni ya fedha watu hawasemi lolote?” Alihoji Bana na kuongeza:

“Watanzania wasimhukumu mtu kwa hisia, sidhani kama hata hiyo kamati yake ina watu wasafi…, Lowassa kisheria na kisiasa yuko safi ila kihisia si safi, tunatakiwa kufanyia kazi hali halisi si hisia,”.
Hata hivyo, alisema pamoja na Bunge kupeleka suala hilo kwa kamati inayoongozwa na Lowassa, Serikali pia inaweza kuunda tume yake ya kuchunguza ufisadi huo.

Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Bashiru Ally alisema kuwa unyeti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama unaweza kufanya majibu ya uchunguzi huo yakawa wazi au kuwa siri.

“Wanaweza kusema kuna mambo hawawezi kuyasema kwa ajili ya usalama wa nchi, ila binafsi nilidhani suala hili lingepelekwa Kamati ya Nishati na Madini au ile ya Mashirika ya Umma, sijui Spika wa Bunge katumia vigezo gani kulipeleka suala hili katika kamati hii,” alihoji Bashiru. Habari hii chanzo ni Mwananchi.co.tz

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...