Send to a friend Mshambuliaji wa Yanga, Davis Mwape akimtoka beki wa Coastal Union, Mbwana Hamis wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda mabao 5-0. Picha na Jackson Odoyo. Sosthenes Nyoni MSHAMBULIAJI Kenneth Asamoah alifunga mabao mawili na kuiongoza Yanga kuwasambaratisha vibonde wa ligi Coastal Union kwa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabingwa hao waliopoteza mvuto kwa mashabiki wao kutokana na kuanza ligi kwa kusuasua jana walionekana tofauti kabisa kwani katika dakika ya nne mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ghana, Asamoah alifunga bao la kwanza kabla ya Shamte Ally, Davies Mwape, Nurdin Bakari na Mghana huyo kufunga kalamu hiyo ya kishindo. Kiungo Idrisa Rajabu alitoa mchango mkubwa kwenye mauaji hayo kwa kutengeneza mabao matatu kati ya matano ikiwa ni mechi yake ya tatu kuanza kuitumikia Yanga. Umakini huo wa safu ya ushambuliaji ya Ya...