MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WIZARA YA MAMBO YA NDANI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012. Mheshimiwa Godbless Lema Mbunge Jimbo la Arusha Mjini -Chadema --- UTANGULIZI -- Mheshimiwa Spika, kwa maslahi ya umma wa Watanzania, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwepo hapa leo, kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Kambi rasmi ya Upinzani, kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa mujibu wa kanuni ya 99(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2007. Mheshimiwa Spika, natoa pia shukurani zangu za dhati kwa familia yangu, Mke wangu Neema Lema, watoto wangu, Allbless Lema na Brilliant Lema, na wazazi wangu wote, Mzee Elibariki Jonathan Lema na Mama . Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa wapiga kura wangu wa Jimbo la Arusha Mjini kwa imani yao kwangu. Licha ya vitisho, vipigo na mabomu ya machozi yaliyotawala kampeni na hata siku ya kupiga, kuhesabu ku...