Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika ukumbi Club Maasai, mashabiki hao walisema wameona bora kuzunguka na kundi hilo kwa kuwa limekuwa likiwapa burudani wanayoitaka katika miondoko mbalimbali ya muziki.
“Tunapenda kuwanao Madj hawa wakati wote wanapokuwa wakitumbuiza katika kumbi za disko nchini , kwani imekuwa ni vigumu kuwasahau akilini kutokana na wao kujipanga vizuri na kutuporomoshea nyimbo safi ,”walisema mashabiki hao.
Kwa sasa Madj hao , tayari wameanza kutoa burudani hiyo katika sehemu mbali mbali jijini Dar es Salaam, na kuvutia mashabiki wengi.
Kwa mujibu wa mmoja wa Madj hao, Joseph Namalowe, 'Dj Joe' alisema wamekuwa wakizunguka katika kumbi mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya mashabiki wao waliotapakaa kila kona ya jiji hili.
Kundi hilo la Madj walioamua kujiunga na kutoa burudani hiyo ya aina yake, linaundwa na Dj Tass, Dj Joe, Dj Cavy na Dj Victor.
Comments