ALIYE kuwa msanii na pia mtayarishaji wa muziki kwenye studio ya Backyards marehemu Saimoni Sayi 'Complex' mapema wiki hii sauti yake itaanza kusikika tena katika anga za muziki nchini , kutokana mtayarishaji Samwel Mbwana 'Braton' ambaye kwa sasa ndiye mmiliki wa studio kuanza kusambaza wimbo mpya wa marehemu huyo uitwao 'Utatanishi' .
Ukiwa tayari wimbo umefanyiwa hatua ya tasimini kuwa utakuwa katika hali nzuri ya kupendwa na mashabiki wa muziki baada ya wadau kuwaufanyia tasimini walipoalikwa kuusikiliza katika studio ya Backyards jijijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Blog hii 'Braton' amewataja wasanii walioshiriki kuingiza sauti zao kuwa ni Madee na msanii Chid Benz ambapo kuingiza sauti zao hizo umefanya wimbo huo ulioko katika maadhi ya Hip hop kuwa na mvuto zaidi.
"Marehemu Complex aliyefariki kwa ajali mbaya ya gari, Agust 22 mwaka 2005 , alifariki ukukukiwa na baadhi ya nyimbo amabozo alikuwa amezirekodi sauti na kwasasa sauti hizo ndizo nimezikarabati na kuwatafuta wasanii hao wawili kuimba pamoja ,"alisema Braton.
Tayari wadau wakubwa katika sekta ya muziki wanaeleza tukio hilo kwa kulifananisha na tukio la msanii maarufu wa marekani hayati 2Pac , ambaye ameendelea kupakua nyimbo mpya kwa kipindi hiki ambacho hatukonaye duniani , kupitia kampuni inayo simamia mauzo ya nguli huyo aliye bobea kwa michano huyo.
Comments