Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing (WHC), Dk Fred Msemwa akifafanua jambo wakati akitoa maelezo kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati ilipotembelea na kukagua miradi ya WHC iliyopo Kigamboni Gezaulole na Bunju jijini Dar es salaam. Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) wakikagua Mradi wa WHC iliyopo Kigamboni Gezaulole jijini Dar es Salaam. Baadhi ya nyumba za WHC zilizopo Kigamboni Gezaulole jijini Dar es Salaam. Miradi ya WHC iliyopo B unju B jijini Dar es Salaam. Dar es Salaam. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeitaka Taasisi ya Watumishi Housing (WHC) kuendelea kuwa wabunifu wa kijenga nyumba na kuuza gharama nafuu na kutoa muda wa miaka 25 kwa mkopaji ili aweze kulipa deni lake. Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati kamati hiyo ikifanya ziara ya kukagua miradi ya WHC iliyopo Gezaulole Kigamboni pamoja na Bunju B, Mwenyekiti wa kam...