Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Mashindano ya Michezo ya Majeshi yatakayoanza kuanzia Februari 23 hadi Machi 8 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa jana jijini humo na Menyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) Brigedia Jenerali, Suleiman Mzee ambapo amesema michezo hiyo itashirikisha vikosi kutoka kanda saba za majeshi likiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Uhamiaji, Jeshi la Polisi nchini, Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) na Zimamoto na Uokoaji. “ Mashindano hufanyika kila mwaka tumewaalika wageni wa heshima tunatarajia Balozi Seif Ali Idd kutufungulia mashindano Uwanja wa Uhuru,” amesema Brigedia Jenerali Mzee. Amebainisha kuwa mashindano hayo yatashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo ya mpira wa pete, mpira wa miguu, mpira mikono wanawake na wanaume, Ndondi, mpira wa wavu, kikapu, kulenga shabah...