Daktari Eva Carneiro akionekana kujibizana na Jose Mourinho Daktari wa Chelsea Eva Carneiro ameamua kuondoka klabuni hapo wiki sita baada kukosolewa na kocha Jose Mourinho. Carneiro alidharauliwa na Mourinho ambaye alisema kuwa daktari huyo ni mwoga kwani alimtibu Eden Hazard wakati wa 2-2 dhidi ya Swansea Agosti 8. Mourinho akimpigia kelele Eva Carneiro (hayupo pichani) Chelsea walimuomba Carneiro, 42, arudi kazini, lakini alikataa na sasa anafikiria kuwaburuza mahakamani. Chama cha soka cha Uingereza FA kinachungumza malalamiko kwamba Mourinho alitumia lugha chafu dhidi yake. Eva na Fearn wakijaribu kumtibu Eden Hazard Chelsea wamesema hawazungumzii masuala ya ndani ya timu.