Skip to main content

WEMA, AUNT KICHEKO KABURINI KWA NGWEA


INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au 'waliamka' nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh!
Mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel wakiangusha kicheko katika kaburi la marehemu Albert Mangweha 'Ngwea'.
Lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel walionesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha 'Ngwea' na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo.
ENEO LA TUKIO
Tukio hilo lililonaswa zimazima na kamera za Risasi Jumatano, lilijiri Januari Mosi, mwaka huu kwenye kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi ya Kihonda mjini Morogoro.
ILIVYOKUWA
Aunt ndiye aliyeanza kutia timu kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya 'kruu' ya Wema, akiwemo Petit Man nayo ilifika na kuungana na Aunt.Baada ya dakika tatu, Mama la Mama, Wema aliwasili akiwa ndani ya nguo isiyokuwa ya mtoko, akakaa upande wa pili wa kaburi. Yeye na Aunt walikaa kwa kupeana ubavu.
CHA AJABU SASA
Awali ilidaiwa kuwa, kruu hiyo ilipanga kuwa baada ya kufika kwenye kaburi hilo wangefanya dua fupi kwa ajili ya kumwombea marehemu apumzike kwa amani huko aliko.Lakini cha ajabu, kabla ya ibada hiyo, Wema, Aunt na wafuasi wao walikuwa wakipiga stori za hapa na pale na katika hali ya kushangaza zaidi, ilifika mahali wakaanza kucheka kile kicheko cha kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio hili kujua nini hasa kilichokuwa kikiwachekesha!
...Wakizidi kucheka katika kaburi hilo.
Baadhi ya wapita njia waliokuwa wakikatiza karibu na makaburi hayo, nao walipigwa na butwaa kuwaona watu hao, walioamini ni ndugu wa marehemu, wakiangua vicheko kama hawana akili nzuri. kwa nukta kadhaa walisimama na kushangaa kabla ya kuendelea na 'hamsini zao'.-
WEMA ATUMIA SIMU KUFICHA USO
Ni dhahiri kuwa, Wema alijishtukia kuwa kitendo cha kucheka juu ya kaburi hakikuwa na ujazo wa kiungwana hivyo haraka sana aliweka simu sehemu ya midomoni na kumfanya asionekane kwenye kamera kwamba alikuwa akicheka. Miwani ya jua aliyovaa pia ilimsaidia.
Wakati Wema akionesha ubinadamu huo, 'mwenzangu na mimi', Aunt yeye alijimalizia kiu yake ya kicheko mpaka pale alipoamua mwenyewe kuacha na si kwa kuogopa kamera wala malaika waliolizunguka kaburi lile (kama wapo) la mmoja wa marapa bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania.
WEMA AJIELEZA KWA RISASI
Baada ya wote kuacha kucheka na kila mmoja kuchukua nafasi ya ubinadamu, paparazi wetu alimuuliza Wema ni kwa nini walionesha kuwa na furaha juu ya kaburi la staa huyo.Wema: "Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na rafiki yetu Mangweha hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo."Ishu ya kupiga stori na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo kaburini, maana kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa sababu tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu."
Albert Mangweha 'Ngwea' enzi za uhai wake.
KWA NINI WALIFANYA ZIARA KABURINI KWA NGWEA?
Awali, mastaa hao na wapambe wao walikuwa na shoo ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika Desemba 31, 2014 ndani ya Ukumbi wa Matei Lounge mjini Dodoma.Wakiwa wanarudi Dar, walipiga kituo mjini Morogoro ambapo miongoni mwa mambo waliyokuwa nayo kwenye ratiba ni kulitembelea kaburi la Ngwea na kuangusha dua fupi.
Hata hivyo, baada ya yote hayo, kundi hilo la Wema na watu wake hatimaye walifanya dua fupi ya kumuombea malazi mema Albert Mangweha.
KUMBUKUMBU MUHIMU
Mangweha alikuwa msanii wa Bongo Fleva. Akiwa na miaka 31 alifariki dunia, Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini. Chanzo cha kifo chake inadaiwa ni matumizi yaliyopitiliza ya madawa ya kulevya. Alizikwa Morogoro, Tanzania, Juni 6, 2013.
CHANZO:GLOBALPUBLISHERS

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...