Mbunge wa
Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya
Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na
kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni.
SHULE ya
msingi Kibindu,Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,ipo hatarini
kufungiwa kutokana na vyumba vya madarasa kuanguka na miundombinu yake
kuwa chakavu hivyo kuhofiwa kuhatarisha maisha ya wanafunzi na walimu.
Aidha
shule hiyo imekuwa ikiezuliwa baadhi ya majengo yake mara kwa mara
kutokana na kutofanyiwa ukarabati tangu shule hiyo ijengwe zaidi ya
miaka 50 iliyopita.
Kutokana
na hali hiyo wanafunzi wa shule hiyo wanakabiliwa na ukosefu wa vyumba
vya madarasa vilivyo bora na imara hali inayosababisha wanafunzi 200
kulundikana katika chumba kimoja.
Akizungumzia
hali hiyo mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae yupo
katika ziara ya siku 10 jimboni humo akitembelea maeneo mbalimbali
ikiwemo shule hiyo ambayo baadhi ya majengo yake yameanguka ,alisema
hayuko tayar kushuhudia wanafunzi wakiendelea kusoma katika mazingira ya
hatari.
Ridhiwani
alilazimika kutoa kauli hiyo baada ya kukagua madarasa hayo na
kushuhudia vyumba vinne vinavyotumika kuwa hatarini kubomoka kutokana na
kutawaliwa na nyufa.
"Nimesikitishwa
sana na ningekuwa na uwezo ningeifunga hii shule isitumike kwani shule
inafunguliwa tarehe 14 mwezi huu ,wanafunzi watakuja kusomea wapi
,wakati pia majengo yaliyobakia yanaweza kuanguka wakati wowowte pia,ni
lazima juhudi za lazima zifanyike kuokoa maisha ya wanafunzi hawa"
alisema Mbunge huyo.
Ridhiwani
alisema kuwa atawsiliana na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Bagamoyo Ibrahim Matovu ili waone ni namna gani wataweza kuelekeza nguvu
zao katika shule hiyo ili iwe katika mazingira bora .
Diwani wa
kata ya Kibindu Mawazo Mkufya alisema taarifa za uchakavu wa
miundombinu ya shule hiyo tayari amezifikisha ngazi ya halmashauri,
ambapo nae kwa upande wake aliomba shule hiyo ifungiwe ili ukarabati
ufanyike
Mtendaji
wa kijiji Cha Kibindu Juma Mgaza, alisema shule hiyo ina matatizo ya
kuezuliwa mara kwa mara wakati wa mvua kutokana na miundombinu yake kuwa
chakavu.
Mgaza aliitaka halmashauri ya wilaya hiyo kufanyia kazi changamoto hiyo kubwa ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi.
Shule ya
msingi Kibindu kwa sasa ina wanafunzi 907 wa darasa la kwanza hadi la
saba ambao wanatarajia kuanza mhula wa masomo kwa mwaka 2015 wiki ijayo
huku ikiwa na vyumba vinne kati ya 14 vinavyohitajika.
Mbali ya
hayo vyumba vya madarasa vimeanguka na vingine vimeweka nyufa kubwa
ambazo zinahofiwa kuanguka wakati wowowte na kusababisha athari kwa
wanafunzi na walimu.VICTOR SIMON
Comments