Maafisa
nchini Nigeria wanasema kuwa kundi la Boko Haram limeuteka mji na kambi
moja ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa kimataifa wanaojaribu
kukabiliana na wapiganaji hao.
Seneta wa Borno Kazkazini Maina
Ma'aji Lawan,eneo la mji wa Baga amesema kuwa wanajeshi waliitoroka
kambi yao baada ya kushambuliwa na Boko Haram jumamosi asubuhi.
Wakaazi wa Baga,ambao walitoroka kupitia maboti hadi taifa jirani la Chad,amesema kuwa raia wengi wameuawa na mji huo kuchomwa.BBC.
Comments