Masharti
mapya yamewekwa na mamlaka ya Lebanon kwa Raia wa Syria wanaoingia
nchini humo , wakati huu ambapo nchi hiyo inapokea Wakimbizi wengi.
Kwa
mara ya kwanza, Raia wa Syria watalazimika kuwa na vielelezo
vinavyoeleza kwa nini wanataka kuvuka mpaka na kuingia nchini Lebanon.
Masharti
haya mapya yanaanza kutumika siku ya jumatatu.Awali kusafiri kati ya
nchi hizo mbili kwa kiasi kikubwa hakukuwa na kikwazo lakini sasa Raia
wa Syria lazima wawe na Viza.
Hatua hii inaelezwa kulenga
kudhibiti idadi kubwa ya Wakimbizi wanaoingia nchini Lebanon, ambapo kwa
sasa Lebanon ina wakimbizi zaidi ya milioni moja.
Hatua hii ya
sasa haijulikani italeta athari gani kwa Raia wengi wa Syria walio
nchini Lebanon ambao hawajajiandikisha kuwa wakimbizi.
Kabla ya
sasa, Raia wa Syria waliweza kukaa nchini Lebanon mpaka miezi sita,
lakini sasa raia wa nchi hiyo watalazimika kutimiza vigezo kadhaa ili
kupatiwa Viza mpakani.Source BBC Swahili.
Comments