Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2015

..Na Uwe Kondakta Wa Basi La Wanyonge...

Uwashushe abiria matajiri wachache wenye kudhamiria kuhujumu safari ya wanyonge walio wengi kwenda kujikomboa kutoka kwenye umasikini. Na matajiri hao wana hila, wanaweza hata kukuhonga kondakta wetu, kwa kwa kuwa tayari hata kukupa nauli zaidi ya uliyopanga kondakta wetu...! Goodmorning. Imeandikwa kwa  Maggid.

MADAI YA KUBEBA UNGA: RAY C AJISALIMISHA POLISI

BAADA ya kukiri kwa mdomo wake kutumia madawa ya kulevya 'unga' na baadaye 'kustaafu', madawa hayohayo yamemletea msanii Rehema Chalamila 'Ray C' 'msala' ambao umemfanya yeye mwenyewe, kwa hiyari yake ajisalimishe polisi. KAWE DARAJANI Chanzo hicho kilinyetisha kwamba, siku ya tukio, wakati Ray C akitokea nyumbani kwake, alipofika maeneo ya Kawe Darajani aliona pikipiki ikimfukuzia na baadaye ikampita na 'kumbloku'. Ilisemekana kwamba baada ya kusimama, jamaa alishuka kwenye pikipiki kisha akamwambia aegeshe pembeni gari lake aina ya Toyota Carina TI. Chanzo kilidai kwamba, Ray C alikataa kufanya hivyo kwa kuhisi aliyekuwa akimwamrisha ni jambazi. "Ray C aliamua kuondoa gari kwa kulazimisha ambapo alimkwepa jamaa huyo kisha kukanyaga mafuta ambapo gari liliondoka kwa kasi," alisema. LUGALO Ilisemekana kwamba baada ya kufika kwenye kituo cha daladala cha Lugalo, a...

JK atema mawaziri 60

Dar es Salaam. Panga pangua ya saba ya Baraza la Mawaziri iliyofanyika juzi imefikisha mawaziri 61 waliotemwa, kujiuzulu au kufariki dunia tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, huku mawaziri 16 wakihimili mawimbi hayo hadi sasa. Katika mabadiliko hayo saba yaliyofanywa katika kipindi cha miaka tisa, wako waliobadilishwa wizara, kupandishwa kutoka naibu waziri kuwa waziri kamili, huku sura mpya zikiingizwa. Mabadiliko hayo yalitokana na mawaziri kutakiwa kuwajibika kutokana na kashfa mbalimbali, huku mengine yakitokana mawaziri kufariki na moja likitokana na Waziri ...

Lema, Nassari wadai watamtoa Muhongo bungeni kwa mabavu

Mbunge wa Arusha mjini (Chadema) Godbless Lema Mbunge wa Arusha mjini (Chadema) Godbless Lema amesema atamtoa kwa mabavu bungeni Waziri wa nishati na madini,Profesa Sospetre Muhongo katika kikao kijacho cha Bunge endapo atakuwa hajaondolewa kwenye nafasi hiyo. Mkakati huo wa Lema umeungwa mkono na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari ambaye pia amepanga kumtoa bungeni kwa nguvu, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge. “Keshokutwa nakwenda bungeni kufanya kazi moja tu, nikimkuta Muhongo bungeni ndipo nitafukuzwa ubunge moja kwa moja,” alisema Lema huku akishangiliwa wananchi na kuongeza; “Nikimkuta Muhongo bungeni na Chenge bado ni viongozi mimi nitakwenda kumshika Muhongo nimtoe bungeni kwa sababu Katiba inaruhusu kila raia kukemea uovu.” Profesa Muhongo na Chenge ni miongoni mwa viongozi ambao Bunge liliazimia wawajibishwe na mamlaka zao kutokana na kashfa ya uchotwaji mamilioni ya fedha katika Akaunti ya T...

150 Duce wapata mimba – Utafiti

Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce). Wanafunzi 150 kati ya 1,000 waliojiunga na masomo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce) mwaka jana wamebainika kuwa na ujauzito waliopewa na wenzao chuoni hapo. Utafiti wa usawa na jinsia uliofanywa na chuo hicho kati ya Juni na Novemba mwaka jana umebaini kuwa wanafunzi wanaopata ujauzito ni wale wa mwaka wa kwanza. Hayo yamebainishwa jana na Mratibu wa Masuala ya Jinsia wa chuo hicho, Dk Dativa Shilla katika warsha ya uchaguzi na uhusiano wa kijinsia iliyofanyika chuoni hapo. Alisema hali hiyo inatokana na kuwapo kwa vitendo vya ukatili, manyanyaso na ubabe unaofanywa na wanachuo wa kiume dhidi ya wale wa kike na hivyo kuwalaz imisha kufanya mapenzi bila hiyari yao. “Kupitia utafiti huu tumeona hakuna usawa wa kijinsia wa kupata elimu baina ya mwanamke na mwanamume kwa sababu mwenye ujauzito hawezi kufanya vizuri katika masomo yake ukilinganisha na mhusika wa kiume,” alisema. Awali, ...

Roc Nation Sports yasimamia Mpambano wa Masumbwi chini ya Jay - Z

Kama 50 Cent alivyojaribu kufanya na bondia Floyd Mayweather, sasa rapa Jay z naye ameanza kusimamia mapambano ya masumbwi na mabondia. Kupitia kampuni yake ya kusimamia maswala ya michezo ya Roc Nation Sports  Jay z amesimamia pambano lake la kwanza. Jay z kama promota amesimamia pambano la Dusty Hernandez “Harisson” alilocheza na Tommy Rainone. Harisson anarekodi nzuri ya kutoshindwa pambano lolote mpaka sasa. Hili ni pambano la kwanza kusimamiwa na Jayz, kuna mengine nane yanakuna na yatakuwa chini ya Roc Nation Sports. Fabolous kama msanii wa Jay z alifanya show  kwenye pambano hili Rihanna alimsindikiza Jay Z kwenye pambano lake la kwanza kama promota  

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo Azindua mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili, mkoani Simiyu ambapo vijiji 170 vimeunganishwa na mradi huo.

 Mwananchi kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) mara Waziri alipotembelea kijiji hicho wakati akielekea kwenye uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili wenye thamani ya shilingi bilioni 25.7.  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima akizungumza na wanakijiji wa Nyanguge wilayani Bariadi juu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme iliyowekwa na REA. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akihutubia wananchi wa kata ya Shishiyu (hawapo pichani) kabla ya kuzindua rasmi mradi wa umeme.  Mtaalamu kutoka kampuni ya LTL (PVT) LTD Michael Marenye akitaja orodha ya vijiji vilivyonufaika na mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili. Kulia ...

BONDIA FLOYD MAYWEATHER AONESHA MALIZAKE NDEGE BINAFSI NA MAGARI LUKUKI

BONDIA Floyd Mayweather wa Marekani amefanya kufuru baada ya kupiga picha akiwa mbele ya ndege yake  binafsi na magari manane ya thamani kubwa anayoyamiliki. Mayweather, anayetajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya pauni milioni 66.1, imeelezwa kuwa thamani ya magari yote manane anayoyamiliki ni pauni milioni tanio. Mbabe huyo wa masumbwi huenda akaingiza mamilioni ya fedha iwapo atakubali kupambana na Manny Pacquiao.

WEMA, AUNT KICHEKO KABURINI KWA NGWEA

INAWEZEKANA ilikuwa utani? Au 'waliamka' nazo?! Kweli binadamu anaweza kuvunjika mbavu (kicheko) juu ya kaburi la mpendwa wake? Mh! Mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel wakiangusha kicheko katika kaburi la marehemu Albert Mangweha 'Ngwea'. Lakini imetokea! Wakati dunia ikisherehekea ujio wa mwaka mpya wa 2015, mastaa wa Bongo, Wema Sepetu na shostito wake, Aunt Ezekiel walionesha jambo tofauti kufuatia kutinga kwenye kaburi la aliyekuwa nyota wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha 'Ngwea' na kutumia muda mwingi kucheka na kutuma meseji kwa simu wakiwa juu ya kaburi hilo. ENEO LA TUKIO Tukio hilo lililonaswa zimazima na kamera za Risasi Jumatano, lilijiri Januari Mosi, mwaka huu kwenye kaburi la Ngwea lililopo katika Makaburi ya Kihonda mjini Morogoro. ILIVYOKUWA Aunt ndiye aliyeanza kutia timu kwenye makaburi hayo na kukaa. Baadhi ya 'kruu' ya Wema, ak...

DMX kuja kivingine

  Kiongozi wa kundi la Ruff Ryders DMX Ametangaza rasmi ujio wa album yake ya nane. DMX Anatoa album iliyopewa jina Redemption of the Beast mnamo January 13, 2015. Info nilizopata mpaka sasa ni kwamba cd itakuwa na nyimbo 16 na wasanii walioshirikishwa ni pamoja na Freeway na msanii mpya Jannyce. Mitaa inazungumzia album mpya ya DMX Kwa kuifananisha na album yake ya kwanza iliyotoka mwaka 1998 “It’s Dark and Hell Is Hot” ambayo ilishika namba moja kwenye chati za album ndani ya wiki moja tu. Hii ndio orodha ya nyimbo kwenye cd hii mpya. Spit That Shit Built Like A Bitch On and On Get Up and Try Again Solid Ft. Rampage I’m Gonna Win It’s A Problem It’s Goin’ Down Shout It One More Night 56 Bars Where You Been Ft. Freeway Right or Wrong Ft. Jannyce Gonna Get Mine We Gonna Make It Love That Bitch Ft. Jannyce

Msanii Diamond kutumbuiza Tuzo za Mwanasoka Bora Afrika 2014

Diamond ameteuliwa kutumbuiza katika tuzo za mwanasoka bora wa Afrika zitakazofanyika jijini Lagos, Nigeria Januari 8, 2015. Msanii Nasib Abdul ‘Diamond’ amechaguliwa kuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kwenye hafla ya utoaji tuzo za mwanasoka bora Afrika 2014.  Diamond atatumbuiza katika tuzo hizo ambazo wachezaji 25 nyota barani Afrika wamechaguliwa kugombea tuzo hizo. Hafla hiyo itafanyika Januari 8, 2015 jijini Lagos Nigeria. Yaya Toure ndiye anayeshikilia tuzo hiyo kwa sasa. Mwanasoka Bora, Yaya Toure raia wa Ivory anayeitumikia Manchester City ya England ni kati ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo. Wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika: Ahmed Musa                          (Nigeria, CSKA Moscow) Asamoah Gyan               ...

Boko Haram lateka kambi ya jeshi Nigeria

Wanajeshi wa serikali waliokuwa wakipiga doria katika mji wa Baga kabla ya Boko haram kuuteka pamoja na kambi ya kijeshi Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa kundi la Boko Haram limeuteka mji na kambi moja ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa kimataifa wanaojaribu kukabiliana na wapiganaji hao. Seneta wa Borno Kazkazini Maina Ma'aji Lawan,eneo la mji wa Baga amesema kuwa wanajeshi waliitoroka kambi yao baada ya kushambuliwa na Boko Haram jumamosi asubuhi. Wakaazi wa Baga,ambao walitoroka kupitia maboti hadi taifa jirani la Chad,amesema kuwa raia wengi wameuawa na mji huo kuchomwa.BBC.

Raia wa Syria wapewa masharti Lebanon

      Lebanon imepokea Wakimbizi zaidi ya Wakimbizi milioni moja kutoka nchini Syria      Masharti mapya yamewekwa na mamlaka ya Lebanon kwa Raia wa Syria wanaoingia nchini humo , wakati huu ambapo nchi hiyo inapokea Wakimbizi wengi. Kwa mara ya kwanza, Raia wa Syria watalazimika kuwa na vielelezo vinavyoeleza kwa nini wanataka kuvuka mpaka na kuingia nchini Lebanon. Masharti haya mapya yanaanza kutumika siku ya jumatatu.Awali kusafiri kati ya nchi hizo mbili kwa kiasi kikubwa hakukuwa na kikwazo lakini sasa Raia wa Syria lazima wawe na Viza. Hatua hii inaelezwa kulenga kudhibiti idadi kubwa ya Wakimbizi wanaoingia nchini Lebanon, ambapo kwa sasa Lebanon ina wakimbizi zaidi ya milioni moja. Hatua hii ya sasa haijulikani italeta athari gani kwa Raia wengi wa Syria walio nchini Lebanon ambao hawajajiandikisha kuwa wakimbizi. Kabla ya sasa, Raia wa Syria waliweza kukaa nchini Lebanon mpaka mie...

SHULE YA MSINGI KIBINDU HATARINI KUFUNGIWA

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. SHULE ya msingi Kibindu,Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,ipo hatarini kufungiwa kutokana na vyumba vya madarasa kuanguka na miundombinu yake kuwa chakavu hivyo kuhofiwa kuhatarisha maisha ya wanafunzi na walimu. Aidha shule hiyo imekuwa ikiezuliwa baadhi ya majengo yake mara kwa mara kutokana na kutofanyiwa ukarabati tangu shule hiyo ijengwe zaidi ya miaka 50 iliyopita. Kutokana na hali hiyo wanafunzi wa shule hiyo wanakabiliwa na ukosefu wa vyumba vya madarasa vilivyo bora na imara hali inayosababisha wanafunzi 200 kulundikana katika chumba kimoja. Akizungumzia hali hiyo mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae yupo katika ziara ya siku 10 jimboni humo akitembele...

WAZIRI WA UCHUKUZI AKUTANA NA WAFANYABISHARA .....!

Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe, akisisitiza jambo alipokutana na wafanyabishara wanaotumia bandari ya Dar es Salaam (hawapo pichani), katika ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Award Massawe, akisistiza jambo, wakati Waziri wa Uchukuzi, alipokutana na Wafanyabishara wanaotumia bandari ya Dar es Salaam  katika ofisi za Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.. Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA), Edward John Urio, akisisitiza jambo wakati wa Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe, alipokutana na wafanyabishara wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam, katika ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA)                                                               ...

KUSITISHA USHUSHWAJI WA BEI ZA FILAMU KWA KAMPUNI YA STEPS

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment. wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya filamu. Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara. IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.