- Huu ndio mwaka ambao kwa mara ya kwanza Totti alivaa jezi ya As Roma na kuanza kucheza soka, alikuwa kijana mdogo wa umri wa miaka 16 tu na mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Italia ulikuwa dhidi ya Brescia ambapo Roma walishinda kwa mabao 2 kwa 0.
1998.Alikuwa na umri wa miaka 21 tu na akaweka rekodi ya kijana mdogo
wa kwanza kupewa cheo cha unahodha wa timu ya As Roma kwa mara ya
kwanza kabisa.
2001.Huu ndio mwaka ambao Totti alibeba ubingwa wa ligi kuu Italia
Serie A na huu ulikuwa ubingwa wake wa kwanza na wa mwisho wa ligi hiyo
nchini Italia,akifunga goli katika ushindi wa mwisho wa 3 kwa 1 dhidi ya
Parma.
2004.Alivunja rekodi ya Roberto Pruzzo ya ufungaji wa muda wote
katika klabu ya As Roma baada ya kufikisha jumla ya mabao 169 na kuwa
mfungaji bora wa muda wote katika klabu hiyo.
2006.Alicheza michezo yote 7 ya timu ya taifa katika kombe la dunia
huku akifunga bao moja na kutoa assists zaidi ya tatu katika michuano
hiyo mikubwa duniani.
2007.Alishinda tuzo ya kiatu cha dhahabu katika ligi kuu nchini
Italia akiwa amefunga mabao 26 katika ligi hiyo huku mabao 32 akiwa
amefunga katika michuano yote aliyocheza msimu huo.
2014.Aliweka rekodi ya mchezaji mkongwe zaidi katika champions league
kufunga goli, kwania alifunga bao la kusawazisha dhidi ya Manchester
City ikiwa ni siku moja tu baada ya kutimiza miaka 38.
2016.Alitokea katika benchi zikiwa zimebaki dakika 5 tu katika mchezo
dhidi ya Torino, wakati anaingia Roma walikuwa wameshapigwa bao 2 kwa 1
lakini akafunga bao mbili na Roma wakamaliza na ushindi wa bak 3 kwa 2.
Comments