Ligi kuu Tanzania bara imehitimishwa leo Mei 20, 2017 kwa mechi zote nane za mwisho kuchezwa katika viwanja tofauti.
Timu tatu za ligi kuu Tanzania bara zimeshuka daraja ambapo msimu ujao zitacheza ligi daraja la kwanza.
JKT Ruvu ilikuwa timu ya kwanza kushuka daraja baada ya kuchapwa na
Toto Africans, JKT Ruvu ikafungwa tena mechi zake mbili za mwisho la
kutupwa ligi daraja la kwanza.
Mechi yao ya mwisho walikua ugenini kucheza dhidi ya Ndanda FC ambayo
pia ilikua inahitaji pointi tatu ili kukwepa mkasi wa kushuka daraja.
Ruvu ikapoteza mechi hiyo kwa kufungwa mabao 2-0.
Toto Africa yenyewe pia ilihitaji ushindi katika mechi ya leo
kuangalia kama inaweza kunusurika na kusalia kwenye ligi kuu Tanzania
bara.
Wakati Toto wakipambana kupata ushindi wakajikuta wakichezea kichapo
cha magoji 3-1 na kushuka daraja hadi ligi daraja la kwanza.
African Lyon nayo imeshuka daraja baada ya kubanwa ugenini na kutoka
suluhu na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Lyon ndio ilikua timu ya kwanza kuifunga Simba msimu huu na kuondoka
na pointi tatu, lakini mambo hayakuwa mazuri kwenye mechi zake za mwisho
za ligi.
Comments