Bado siku chache tu twende Cardiff ambapo pale litapigwa
pambano la kumtafuta mfalme wa michuano ya Champions League msimu huu
kati ya Real Madrid dhidi ya klabu ya Juventus.
Juventus wenyewe wanaelekea katika dimba la Millenium Stadium wakiwa
kikosi chao kiko fiti 100% lakini Real Madrid wenyewe hawako fiti 100%
kutokana na majeruhi muhimu.
Walinzi wao wa kati Pepe na Varane waliumia na hawana uhakika wa kuwa
fiti kabisa kuikabili Juventus lakini huku mshambuliaji wao Gareth Bale
naye akiwa haijulikani kwamba atacheza au vipi.
Kutocheza kwa Gareth Bale kunaweza kuwa jambo jema kwa Juventus kwani
amekuwa mwiba mkali kwa kila timu ambayo inacheza dhidi ya Real Madrid.
Lakini Bale ametuma picha mtandaoni ambayo inaweza kuwanyima raha
mashabiki wasiopenda Real Madrid na kuwakatisha tamaa kuhusu hatma ya
yeye kucheza au kutocheza Jumamosi.
Bale ametuma picha akionekana yuko mazoezini akipasha na wenzake hali
inayoashiria kwamba pengine Bale yuko tayari kuikabili Juventus siku ya
Jumamosi.
Real Madrid ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo na wanaingi
katika fainali hiyo kujaribu kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza
kuchukua ubingwa huo mara mbili mfululizo.
Comments