Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema kwamba,ngoma za asili bado zina hadhi na nafasi kubwa katika jamii zetu ingawa kwa maeneo ya mijini mwamko wa sanaa hiyo unaonekana kupungua tofauti na zamani. Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba,ngoma za asili zipo kama kawaida na zimekuwa na nafasi kubwa mikoani ambako zimekuwa zikivuta watu wengi. “Kuna matamasha makubwa ya ngoma za asili kama yale ya Makuya, ya kale yanapokutana na ya sasa, Bujora na Chamwino.Matamasha haya yamekuwa yakivuta watu wengi sana hivyo,dhana kwamba ngoma za asili zimetoweka si sahihi” alisema Materego. Aliongeza kwamba,kinachotokea kwa sasa ni athari za utandawazi kwenye ngoma za asili ambazo zimebadili upepo wa sanaa hiyo maeneo ya mijini lakini akasisitiza kwamba,bado hata maeneo ya mijini kuna vikundi vingi vya ngoma za asili vinavyofanya vizuri. “Utandawa...