WAKAZI wa mkoani morogoro wanatarajia kushuhudia uzindizi wa alabamu mpya ya muziki wa Taarab Novemba27, pale kundi la Jahazi Modern Taarab litakapo poromosha vibao vyake vipya vilivyo ndani ya albamu yao mpya iitwayoDaktari wa Mapenzi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana msemaji waUzinduzi huo Said Mdoe alisema kuwa hadi sasa maandalizi yashoo ya burudani hiyo yanaenda vizuri .
"Tunatazamia wakazi wa mji kasoro bahari watafika kwa wingikushuhudia uzinduzi huo kwani bado tunafikilia mambo mengine yatakayo boresha mafanikio katika burudani hiyo,"alisema Mdoe.
Alisema bendi hiyo inataraji kutumbuiza nyimbo zake mpya kama Daktari wa Mapenzi iliyoibwa na Mzee Yusufu inayobeba jina la albamu nyingine ni Roho mbaya haijengi iliyoimbwa na Mwana hawa Ali , Domokaya ulioimbwa na Abubakar Amigo , Chokochoko mchokoe pweza ulioimbwa na Mariam Amour. Nyimbo nyingine ni Fungu la Mungu Silikosi ulioimbwa na Leila Rashid pampja nawimbo uitwao Ng;ombe wa Masikini Hazai ulioimbwa na Fatma Ali.
Aidha nyimbo za albamu za kundi hilo zilizo tikisa mashabikikatika anga za muziki huo wa Taarabu kutoka kwenye kundi hilo ni pamoja na albamu iliyoitwa Two In One , Kazi ya mungu Haiingiliwi,Tupendane Wabaya Waulizane pamoja na ile iliyoitwa VIP.
Mdoe alisema kuwa Uzinduzi wa albamu hiyo utafanyikatena siku ya pili kwenye mjimkuu wa Tanzania Dodomajumamosi ya Novemba 28 kwenye ukumbi wa Polisi Jamii mkoani humo.
Comments