MSANII wa muziki wa Bongofleva Masiga Alex 'masiga' ,ambaye apoawali alifanya vizuri akiwa ndani ya kundi la 'Bm Love' nakuvuma na wimbo ulioitwa 'Anakundanganya, Anakudanganya huyo' baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu , ameanza hatua nyingine katika muziki kwa kupakua nyimbo mpya.
Akizungumza na Jatida la Maisha hivi karibuni , Alex amesema kuwa kwa sasa ameanzisha kundi jingine ambalo tayari linaundwa na wasanii watatu .
"Tunakuja na ujio wa albamu yakundi itakayokuwa na nyimbo takribani kumi,"alisema msanii huyo. Alex amewataja wasanii wengine kuwa ni Leah Mud aliye ibiliwa kipaji chake kwenye Bongostar Seach pamoja na Siz - Q ambapo nyimbo tatu tayari zimeishaanzakusambazwa kwenye stesheni mbalimbali za Redio hapa nchini.
Aidha msanii huyo alizitaja nyimbo hizo kuwa ni wimbo wa 'Penzi langu' ulioimbwa na Reah Mud , 'Zumu zumu Zumu' ulioimbwa na Siz - Q na wimbo uitwao 'Mshikaji' ukiwa umeibwa na Masiga.
Masiga ambaye kwa sasa ni Afisa utawala (Offece Adiministrator), wa Kampuni ya Tigo ,jijini Dar es Slaam alitaja jina la albamu hiyo kuwa itaitwa 'Wakweli Projecti One'.
Comments