MSANII wa muziki wa Bongofleva Maurid Pepe 'AM' ameanza hatua ya kukamilisha albamu kwa ajili ya ujio mpya , ambapo tayari amekamilisha nyimbo takribani nne zenye majina ya 'Longo Longo' 'Sina noma' , 'Sema' , pamoja na mwingine uitwao 'Usiondoke'.
Akizungumza na Jarida la Maisha sikuchache zilizopita msanii Pepe alisema kuwa uono mwanzo wa matayalisho kwa ajili ya ujio wa alibamu yao mapema mwakani.
"Haya ni mafanikio yanayoonesha kuleta njia ya kuyafikia mafanikio mapya kwa siku za usoni;"alesema Pepe.
Msanii huyo ambaye amemtaja msanii mwingine aitwaye Hassan Omari kuwa ni mmoja ya msanii muhimu kwake kwani atashiriki nyimbo nyingi studio na tayari ameisha shirikiana naye kwenye vyimbo hizo za awali, zilizo rekodiwa katika studio za Imotion Records , OM Studio na G-2 chini ya produza Roi.
Pichani kama tulivyo mkuta akienda kumjulia hali babake katka Hospitali ya Mwananyamala.
Comments