Hali ya kiafya ya watu ambao wanavuta
sigara inazidi kuwa mbaya baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutoa
ripoti ambayo inaonyesha hivi karibuni kutakuwa na watu milioni nane
ambao watakuwa wanakufa kila mwaka kwa sababu ya uvutaji sigara.
Vifo hivyo vimeripotiwa kuwa vitakuwa
vikitokana na magonjwa ambayo watumiaji wa sigara wanakuwa nayo kutokana
na matumizi ya sigara kuonekana kuongezeka ambapo kwasasa inakadiriwa
kuwa zaidi ya Dola Trilioni moja kutumika kila mwaka kwa ajili ya
kununua sigara.
“Vifo vya watu ambao wanatumia
bidhaa ambazo zinatokana na tumbaku itapanda kutoka watu milioni sita
hadi milioni nane ifikapo 2030, nchi ambazo zitaathirika zaidi ni zenye
uchumi mdogo na wa kati,” ilisema ripoti hiyo.
Wataalamu wa afya wanasema kuwa bidhaa
za tumbaku ni moja ya vitu hatari kwa afya na ambavyo vimekuwa
vikisababisha vifo vya watu wengi lakini bado idadi ya watumiaji wake
inazidi kuongezeka kwa kasi katika maeneo mbalimbali duniani.
Comments