· Asema kazi ndio imeanza.
· Atoboa siri ya ushindi wake…. Wingi wa wenzetu unawabeba!
WAWAKILISHI wa Tanzania katika mbio za 14 za Standard Chartered Mumbai Marathon Alphonce Simbu na mwanadada Magdalena Krispin,wamewasili nchini jana nakueleza furaha
ya ushindi.
Simbu akiwa mwenye furaha alitoboa siri nzito kuhusu ushindi wake ambapo alichukua nafasi ya kwanza akimtimulia vumbi mpinzani wake wa karibu Mkenya Joshua Kipkorir katika kundi la wakimbiaji wa nje.
Akizungumza mara baada ya kuwasili,Simbu alianza kwa kutoa shukrani kubwa kwa Watanzania wote ambao wamekuwa wakimuombea na kumtakia kila la heri.
“Kwa kweli nimefurahi sana kwa ushindi huu na siri kubwa ya ushindi wangu nikujituma na nawashukuru udhamini kutoka Multichoice Tanzania,"alisema .
Comments