Mkurugenzi na mmliki wa bendi kongwe ya muziki wa dansi
nchini Twanga Pepeta, Asha Baraka amedai yupo mbioni kuachana na maswala
ya muziki na kujikita kwenye siasa.
Asha Baraka
Asha Baraka amedai tayari ameshafanya kazi kubwa kwenye muziki wa
dansi na muda huu ni kwa ajili ya vijana na yeye aingie kwenye siasa.
“Muziki unakuwa kwa kasi sana japo kuwa bado kuna changamoto nyingi
kama unavyojua, media nyingi hazipigi nyimbo za muziki wa bendi kwa
uwiano sawa na nyimbo za aina zingine za muziki. Kwa hiyo media
zibadilike kwa sababu sisi wengine tunajipanga kuwaachia vijana na
kuingia kwenye siasa,” Asha Baraka alikiambia kipindi cha NFL cha EATV.
Pia alisema anaamini wizara yenye dhamana na maswala ya burudani
itafanya juhudi za kusaidia kuurudisha muziki wa dansi katika chati kwa
mwaka 2017.
Comments