Mfanyabiashara maarufu, Mustafa Jaffar Sabodo
Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere
Aliyekuwa Kiongozi wa Taifa la Iran, Ayatolah Khomein
Mwandishi Wetu
HAKIKA ukitaja jina la Mustafa Jaffer Sabodo, siyo geni masikioni mwa Watazania wengi.
Hii ni kutokana na mchango wake kwa jamii katika kuliondoa taifa kutoka sehemu moja ya chini kwenda juu, yaani maendeleo.
Sabodo
mfanyabiashara maarufu ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Asia amekuwa
akitoa mchango kwa maendeleo ya Taifa katika nyanja mbalimbali kuanzia
za uchumi, siasa, elimu, afya na maji.
Mfanyabiashara
huyo ambaye ni mzaliwa wa mkoani Lindi takriban miaka 73 iliyopita
amejitolea kujenga shule mbalimbali nchini, hospitali, visima vya maji
hata kufadhili shughuli za kisiasa na kiuchumi.
Michango
yake hiyo kwa jamii ya Watanzania, imefanya jina lake kuandikwa katika
mioyo ya wananchi wengi kwani alidhirisha tabia yake isiyojificha ya
uzalendo kwa Taifa lake Tanzania.
Sabodo anatajwa kuwahi kuvifadhili vyama vya siasa vya CCM na Chadema kwa nyakati tofauti.
Pia
anatajwa kwamba alikuwa rafiki wa karibu wa Mwalimu Julius Nyerere na
wanasiasa mbalimbali nchini hata kuwahi kutumwa kwenda nchini Iran
kukutana na kuomba mafuta kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo la
Kiislamu, Ayatolah Khomein katika miaka ya 1970 baada ya taifa kukumbwa
na uhaba wa mafuta uliochagizwa na sababu mbalimbali ikiwamo ukosefu wa
fedha za kigeni.
Hali
hiyo ilitokea kipindi hicho wakati dunia ilikuwa bado ikishuhudia
mgawanyiko kwa baadhi ya nchi kuegemea Marekani kisiasa na kimfumo,
nyingine zikifuata mfumo wa iliyokuwa Muungano wa nchi za Kisovieti za
Urusi (USSR).
Si
hivyo tu kwa kusoma alama za nyakati, baadhi ya nchi zilikaa kando na
utengano huo na kuanzisha Jumuia ya Nchi Zisizofungamana na Upande
Wowote.
Miungoni
mwa mataifa yaliyofuata siasa za kutofungamana na upande wowote,
Tanzania wakati huo chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere ilikuwa mojawapo.
Tofauti
hizo za kisiasa hata kidini kati ya mataifa zilisababisha athari
zilizozaa tofauti ya hali hasa kiuchumi na kisiasa hata baadhi ya nchi
kuingia kwenye mahangaiko ikiwamo Tanzania iliyokumbwa na uhaba wa
mafuta ya Petroli na fedha za kigeni.
Sabodo
anasimulia kwamba kufuatia hali hiyo iliyoilazimu Serikali kuzuia
magari yake kutembea Jumapili huku Jumamosi yakitembea hadi saa nane
mchana, alipata nafasi ya kukutana na Rais Nyerere.
Anasimulia kwamba katika mazungumzo hayo alimwabia Rais Nyerere haja yake ya kutaka kwenda Iran kuomba mafuta.
“Nikamwambia
wacha niende Iran. Nilifanya hivyo nikiamini Khomein atanisikiliza.
Nakumbuka nilikwenda na Chifu Adam Sapi Mkwawa,” anasema.
Anasimulia:
“Mimi ni Khoja, Mwislamu wa dhehebu la Shia na Khomein pia,
nilipokutana naye, nikamwambia wanaoteseka Tanzania kwa shida ya mafuta
wamo piaWaislamu wa Shia wengi tu.”
“Nilimwambia
Tanzania ni nchi nzuri haina ubaguzi na Rais Nyerere ni mtu mwema, hata
Waziri Mkuu wake ni Rashid Kawawa na Waziri wa Madini na Mafuta ni
Anoor Kassam, nikamwangukia miguuni nikiliaa kuomba aipe nchi yetu
mafuta, akakubali” anakumbuka Sabodo.
Hata
hivyo, anasema licha ya kukubali, Khomein akasema hawezi kumpa mafuta
yeye Sabodo hadi watu wa Serikali ya Tanzania watakapofika Iran
kuthibitisha ombi hilo.
“Nikarudi
Tanzania na kumpa taarifa baba wa Taifa naye alimwambia Kawawa na John
Malicela ikakubalika tukaenda tena Iran safari hii nikiwa na mawaziri wa
Fedha, Cleopa Msuya, Anoor Kassam wa Mafuta na Usafirishaji pia
alikuwepo Peter Noni kwa niaba ya Benki Kuu na Adam Sapi Mkwawa,”
anasema.
Sabodo
anakumbuka kuwa safari hiyo ilizaa matunda kwani Khomein aliipa
Tanzania mafuta yenye thamani ya Dola za Kimarekani 80,000.
“Nakumbuka
hapo urafiki wangu na Nyerere uliniwezesha kuliokoa Taifa kwa kupata
mafuta baada ya kunituma kwenda Iran nilipomshauri,” anasema Sabodo
ambaye wazazi wake alizaliwa Lindi.
Anakumbuka
kuwa pia katika safari hiyo alimshauri Khomein kufungua ofisi ya
Ubalozi wa Iran nchini naye alikubali na alifanya hiyo pia kwa Zambia,
Tanzania nayo ikafungua ubalozi Iran.
Don’t forget to read my book; CORRUPTION IS CRUCIFICATION OF TANZANIA, which is in process(P.T) .Inatoka http://www.mjengwablog.com/
Comments