Waziri wa
Habari, utamaduni, michezo na sanaa Kushoto,Diamond Platnumz katika
pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania bw.Salum Salum.
Afisa
Masoko wa Multichoice Tanzania Shumbana Walwa akiwa anaongea na
waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kumkabidhi Diamond Platnumz
bendera ya Tanzania kuelekea katika ufunguzi wa Afcon nchini Gabon.
Meneja
Masoko wa Multichoice Tanzania Bw.Alpha Joseph akimkalibisha Kaimu
Mkurugenzi Salum Salum katika hafla ya utoaji wa Bendera kwa msanii wa
Bongo Fleva Diamond Platnumz.
Kaimu
Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Bw.Salum Salum akimkaribisha mgeni wa
tukio ambaye ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Mh.Nape
Nnauye hayupo pichani.
Waziri wa
Habri,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh.Nape Nnauye akiongea na waandishi
wa habari wakati wa kumkabidhi Bendera Diamond Platnumz anayekwenda
kwenye shoo ya Ufunguzi wa Afcon nchini Gabon.
Msanii
Diamond Platnumz akitoa shukruni kwa Serikali na DStv pamoja na
waandishi wa habari kwa mchango wao pamoja na kuendelea kumsapoti
kupitia kazi zake.
Mh.Nape Nnauye akisalimiana na Msanii Diamond Platinum.
Msanii wa
vichekesho nchini Tanzania JOTI ambaye pia ni balozi wa Kifurushi cha
DStv Bomba ambacho kitarusha moja kwa moja Michuano ya Afcon akitoa
pongezi kwa Kampuni ya Multichoice Tanzania.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Mh.Nape Nnauye katika akiwa na balozi
wa kifurushi cha Bomba Joti kulia pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa
Multichoice Tanzania Bw.Salum Salum kushoto wakiteta jambo.
Baadhi ya Waandishi waliohudhuria tukio hilo wakiwa katika majukumu yao ya kuchukua picha.
Msanii
Diamond Platinum akiwa na bendera baada ya kukabidhiwa na Serikali
tayari kuelekea kwenye ufunguzi wa Michuano ya Afcon inayoanza Jumamosi
ya Januari 14.
Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Nape Nnauye pamoja na Msanii Diamond Platinum.
PICHA NA MO DEWJIBLOG.
Kuelekea
katika Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika ‘AFCON’
Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia Kifurushi cha DStv Bomba imetoa
tiketi sita kwa vijana wa Msanii wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul ‘Diamond
Platinum kwenda kushuhudia ufunguzi huo.
Ufunguzi
huo wa michuano hiyo mikubwa Afrika, inatarajiwa kufanyika Januari 14,
mwaka nchini huko ambako Dimaond amealikwa kwenda kutuimbuza.
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimkabidhi bendera ya
taifa, Diamond kwa ajili ya kwenda kuipeperusha vyema Tanzania katika
ufunguzi huo.
“Kikuweli
nimpongeze Diamond kwa mwaliko alioupata wa kwenda kutumbuiza kwenye
michuano mikubwa Afrika ya Afcon, siyo kitu kidogo kwake, ni nafasi ya
yeye kujitangaza zaidi kimataifa, ninaamini wapo wasanii wengi wazuri
Afrika, lakini kachaguliwa yeye hivyo anastaili pongezi,” alisema Nape.
Nape
ndiye aliwaomba DStv kujitokeza na kudhamini safari ya wachezaji shoo wa
Diamond na baadhi ya watu wa timu yake kwenda Afcon ili kuhakikisha
anafanya shoo ya uhakika zaidi.Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DStv, Salum Salum
alisema wametoa tiketi hizo kwa Diamond kwa lengo kukuza na kuendeleza
vema tasnia ya filamu.“Tunathamini
tasnia ya sanaa nchini kwa kupitia muziki na filamu, hivyo basi katika
kutambua hilo tumetoa tiketi sita kwa kundi la WCB chini ya msanii
Dimaond kwa ajili ya kwenda kwenye uzunduzi wa Afcon huko Gabon.
“Tumempatia
tiketi hizo, baada ya kuomba udhamini wa tiketi hizo kwa ajili ya
vijana wake sita atakaombatana nao kwenye shoo hiyo na kikubwa tunataka
kuona Diamond anafunika ili atauwakirishe vema,” alisema Salum.DStv,
ndiyo itaonyesha michuano hiyo mikubwa ya kimataifa kwa kifurushi chake
cha bei cha chini kabisa kitakachopatikana kwa Shilingi 19, 975 tu.(P.T)
Comments