Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2017

Shujaa Alphonce Simbu atua nchini!

· Asema kazi ndio imeanza. · Atoboa siri ya ushindi wake…. Wingi wa wenzetu unawabeba! WAWAKILISHI wa Tanzania katika mbio za 14 za Standard Chartered Mumbai Marathon Alphonce Simbu na mwanadada Magdalena Krispin,wamewasili nchini jana nakueleza furaha ya ushindi. Simbu akiwa mwenye furaha alitoboa siri nzito kuhusu ushindi wake ambapo alichukua nafasi ya kwanza akimtimulia vumbi mpinzani wake wa karibu Mkenya Joshua Kipkorir katika kundi la wakimbiaji wa nje. Akizungumza mara baada ya kuwasili,Simbu alianza kwa kutoa shukrani kubwa kwa Watanzania wote ambao wamekuwa wakimuombea na kumtakia kila la heri. “Kwa kweli nimefurahi sana kwa ushindi huu na siri kubwa ya ushindi wangu nikujituma na nawashukuru udhamini kutoka Multichoice Tanzania,"alisema .

KAMATI YA UTENDAJI YA CAF IMEFIKIA HAPA KUHUSU MCHEZAJI LANGA LESSE BERCY

Langa Lesse Bercy Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF), limetoa nafasi ya mwisho kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Congo (FECOFOOT) kumpeleka mchezaji Langa Lesse Bercy jijini Libreville, Gabon kwa ajili ya kipimo kipya cha MRI ili kutambua umri wake. CAF limetaka FECOFOOT kumpeleka mchezaji huyo huko Libreville, Gabon ndani ya siku 10 zijazo kuanzia jana Januari 12, 2017. CAF limepata kumwita mchezaji huyo mara mbili mwaka jana, na FECOFOOT imeshindwa kumpeleka kwa sababu mbalimbali wanazozijua FECOFOOT. Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya kimataifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, vijana waliohitajika kucheza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 17. Langa Lesse Bercy, amelalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwamba amezidi umri hivyo kuhitajika kumpeleka kwani hakustahili kucheza hatua ya kufuzu kwa michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya A...

R. Kelly - The Storm Is Over Now - YouTube

KUFUZU AFCON 2019

Group L ------------- Cape Verde Uganda Tanzania Lesotho Na hapa tutashindwa?   Baada ya kusota kwa miaka kadhaa timu ya taifa ya Tanzania ‘Stars’kupangwa kwenye makundi magumu hatimaye CAF imeipa ahueni na kuipanga katika kundi L, kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon pamoja na Uganda, Cape Verde na Lesotho. Hili linaweza kuwa kundi rahisi zaidi Taifa Stars, kwani zote Uganda, Cape Verde na Lesotho ni timu ambazo zipo ndani ya uwezo wake – kikubwa ni maandalizi ni mshikamano wa Watanzania kama taifa. Kenya pia itaanzia hatua ya makundi, ikiwa imepangwa Kundi F pamoja na Ghana, Ethiopia na Serra Leone, wakati Rwanda ipo Kundi H pamoja na Ivory Coast, Guinea na Afrika ya Kati (CAR). Mshindi wa kila kundi atafuzu moja kwa moja AFCON ya 2019, wakati timu nyingine tatu zitakazomaliza nafasi ya pili na wastani mzuri zaidi ya nyingine zitafuzu kama washindi wa pili bora. Michuano hiyo itaanzia kwa hatua ya mchujo, Raundi ya Awali...

TBBF yatoa ongera kwa Mapinduzi Day jana

watu wanaokufa kwa uvutaji wa sigara kuongezeka hadi watu milioni 8 kwa mwaka

Hali ya kiafya ya watu ambao wanavuta sigara inazidi kuwa mbaya baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutoa ripoti ambayo inaonyesha hivi karibuni kutakuwa na watu milioni nane ambao watakuwa wanakufa kila mwaka kwa sababu ya uvutaji sigara. Vifo hivyo vimeripotiwa kuwa vitakuwa vikitokana na magonjwa ambayo watumiaji wa sigara wanakuwa nayo kutokana na matumizi ya sigara kuonekana kuongezeka ambapo kwasasa inakadiriwa kuwa zaidi ya Dola Trilioni moja kutumika kila mwaka kwa ajili ya kununua sigara. “Vifo vya watu ambao wanatumia bidhaa ambazo zinatokana na tumbaku itapanda kutoka watu milioni sita hadi milioni nane ifikapo 2030, nchi ambazo zitaathirika zaidi ni zenye uchumi mdogo na wa kati,” ilisema ripoti hiyo. Wataalamu wa afya wanasema kuwa bidhaa za tumbaku ni moja ya vitu hatari kwa afya na ambavyo vimekuwa vikisababisha vifo vya watu wengi lakini bado idadi ya watumiaji wake inazidi kuongezeka kwa kasi katika maeneo mbalimbali duniani.

Msome Mjengwa na Simulizi Za Kusisimua jinsi Mobutu alipokodi ndege ya wachawi

UGANDA, YAPIGWA 3-0

KIPA namba moja wa Uganda, Denis Onyango aliumia jana wakati timu yake ikifungwa mabao 3-0 na na mabingwa wa Afrika, Ivory Coast katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Chuo Kikuu cha New York mjini Abu Dhabi. Pamoja na hayo, Onyango anatarajiwa kuwa fiti kabla ya mchezo wa kwanza wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya  Ghana Januari 17  Uwanja wa Port Gentil, Gabon. Kipa huyo wa Mamelodi Sundowns alianguka dakika ya 38 baada ya kuumia nyonga ya mguu wa kushoto . Hata hivyo, akapatiwa matibabu na kurudi kumalizia dakika 45 za kipindi cha kwanza timu zikirudi vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa hazijafungana, lakini mwanzoni mwa kipindi cha pili msaidizi wake, Robert Odongkara akachukua nafasi. Denis Onyango aliumia jana na kuiacha Uganda ikifungwa mabao 3-0 na Ivory Coast katika mchezo wa kirafiki Abu Dhabi Na Ivory Coast wakafanikiwa kupata mabao matatu kupitia kwa  Jonathan Kodjia dakika ya 51, Wilfried Zaha dakika ya 58...

Sabodo azungumza :Ukaribu wangu na Mwl. Nyerere uliokoa Taifa

 Mfanyabiashara maarufu, Mustafa Jaffar Sabodo  Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere Aliyekuwa Kiongozi wa Taifa la Iran, Ayatolah Khomein  Mwandishi Wetu HAKIKA ukitaja jina la Mustafa Jaffer Sabodo, siyo geni masikioni mwa Watazania wengi. Hii ni kutokana na mchango wake kwa jamii katika kuliondoa taifa kutoka sehemu moja ya chini kwenda juu, yaani maendeleo. Sabodo mfanyabiashara maarufu ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Asia amekuwa akitoa mchango kwa maendeleo ya Taifa katika nyanja mbalimbali kuanzia za uchumi, siasa, elimu, afya na maji. Mfanyabiashara huyo ambaye ni mzaliwa wa mkoani Lindi takriban miaka 73 iliyopita amejitolea kujenga shule mbalimbali nchini, hospitali, visima vya maji hata kufadhili shughuli za kisiasa na kiuchumi. Michango yake hiyo kwa jamii ya Watanzania, imefanya jina lake kuandikwa kat...

DStv WAONGEZA NGUVU SHOO YA DIAMOND PLATINUM UFUNGUZI WA AFCON NCHINI GABON

Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na sanaa Kushoto,Diamond Platnumz katika pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania bw.Salum Salum. Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania Shumbana Walwa akiwa anaongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kumkabidhi Diamond Platnumz bendera ya Tanzania kuelekea katika ufunguzi wa Afcon nchini Gabon. Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bw.Alpha Joseph akimkalibisha Kaimu Mkurugenzi Salum Salum katika hafla ya utoaji wa Bendera kwa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz. Kaimu Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania Bw.Salum Salum akimkaribisha mgeni wa tukio ambaye ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Mh.Nape Nnauye hayupo pichani. Waziri wa H...

Wolper atumia Instagram kumpiga chini Harmonize

Wasahau tena Jacqueline Wolper na Harmonize aka ‘WoHa’ama vyovyote ulivyokuwa ukiwaita pamoja. Ni kwasababu Wolper amembwaga rasmi hitmaker huyo wa Bado tena kupitia Instagram. Hata hivyo post hiyo haikuweza kukaa kwa muda mrefu – imefutwa, japo wapo waliowahi kuinasa mapema. Kwenye post hiyo iliyokuwa na picha ya Harmonize pamoja na emoji za alama ya kopa iliyopasuka, Wolper ameandika: Nina akili timamu me syo mtoto mdogo, endelea na maisha yako it over waambie rasmi usifiche @harmonize_tz i hate love.” Looks like Harmonize kauvunja moyo wa Wolper kiasi cha kuamua kuyachukia mapenzi kiasi hicho!

Soma hapa Kinachokwamisha Collabo ya Lady Jay Dee na Diamond

Mkongwe katika anga la bongo fleva, mwanadada Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee amesema yuko tayari kufanya kazi na staa wa muziki huo Diamond Platnumz, endapo atahitaji lakini kinachoweza kukwamisha ni ratiba yake ya kazi. Jay Dee amelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na kuongezeka kwa minong'ono kuwa wawili hao wanakwepana, na hawataki kufanya kazi kwa pamoja, ambapo amekuwa akikabiliwa na mambo mengi kwenye ratiba yake. Akiwa katika Kitengo ya Planet Bongo ya EATV, Jay amesema hana tatizo na msanii yoyote nchini na yuko wazi wakati wowote, lakini akasita kutaja ni wakati gani atafanya kazi na Diamond. "Kwa sasa nina ratiba za mambo mengine, lakini akinihitaji niko tayari na tutafanya kazi wakati muafaka nikiwa na na nafasi" Alisema Jay Dee. Mwezi Novemba mwaka jana, Diamond alipozungumza na EATV kuhusu suala hilo alisema yuko tayari kufanya kazi na mwanadada huyo, lakini tatizo ni kubanwa na ratiba ambayo imekuwa haimpi nafasi. Kwa k...

Disco la Flavour Nite Mzalendo Pub latikisa mkesha wa mwaka mpya

 Wadau wajiachia katika kuupokea  mwaka mpya  Flavour Nite  Dar ilivyotikiswa katika mkesha wa mwaka mpya na Dj Mwenye heshima kubwa nchini Bonny Luv Fideline Iranga ajichanganya na ...... katika kuupokea mwaka 2017 ndani ya  Flavour Nite

Asha Baraka:Najipanga kuwaachia vijana muziki niingie kwenye siasa

Mkurugenzi na mmliki wa bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini Twanga Pepeta, Asha Baraka amedai yupo mbioni kuachana na maswala ya muziki na kujikita kwenye siasa. Asha Baraka Asha Baraka amedai tayari ameshafanya kazi kubwa kwenye muziki wa dansi na muda huu ni kwa ajili ya vijana na yeye aingie kwenye siasa. “Muziki unakuwa kwa kasi sana japo kuwa bado kuna changamoto nyingi kama unavyojua, media nyingi hazipigi nyimbo za muziki wa bendi kwa uwiano sawa na nyimbo za aina zingine za muziki. Kwa hiyo media zibadilike kwa sababu sisi wengine tunajipanga kuwaachia vijana na kuingia kwenye siasa,” Asha Baraka alikiambia kipindi cha NFL cha EATV. Pia alisema anaamini wizara yenye dhamana na maswala ya burudani itafanya juhudi za kusaidia kuurudisha muziki wa dansi katika chati kwa mwaka 2017.