Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Ujenzi wa Mwili Tanzania (TBBF) limesema kuwa limeanza kuimiza wanafunzi wa vyo vikuu nchini kujiunga na kushiriki katika shindano la kumsaka Mr.Handsome . TBBF mara baada ya kuwa imezindua shindano hilo hivi karibuni hivi sasa wanafunzi wanaotaka kujiunga kwa kutumia mtandao wa www.tztbbf.org nakisha kubonyeza sehemu ya shindano kuchagua sehemu wanayotaka kushiriki. Akizungumzia hatua ya shindano hilo mmoja wa wasemaji wa shindano hilo Fike Wilson alisema jana kuwa mara baada ya washiriki kuingia katika mtandao huo washiriki wanatakiwa kuandika jina kamili,Anuani , namba ya simu na anuani ya barua pepe. Alisema kama mshiriki atakuwa amefuata maelekezo hayo na kujiandikisha kwa ufasaha basi baadaya atapokea ujumbe kwa njiaya barua pepe aliyoitoa hivyo washiriki wanatakiwa kuhakikisha wametoa anuani sahihi ya barua pepe. "Washiriki wakati wa kutumia parua pepe watatakiwa kuambatanisha...