Marehemu Adam Kuambiana ataagwa siku
ya jumanne (20/5/2014), katika viwanja vya Leaders Club, kuanzia saa 3
asubuhi hadi saa 9 mchana. Baada ya hapo atazikwa siku hiyo hiyo ya
jumanne, katika makaburi ya Kinondoni.
Mwenyekiti wa Bongo movies, Steve
Nyerere, amesema marehemu alikuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo na
ndio chanzo cha kifo chake.
Comments