Na RFI
Serikali ya Mali imetangaza vita dhidi ya “magaidi”, siku mbili baada ya
mapigano makali kutokea katika mji wa Kidal (kaskazini mwa nchi),
ambako ni ngome kuu ya waasi kutoka jamii ya Tuareg.
Kwa mujibu wa serikali ya Mali, maafisa 30 wa serikali wametekwa nyara
na waasi. Kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa, watu wanane
wameuawa.
Makabiliano makali yalitokea kati ya jeshi na makundi ya waasi wakati
waziri mkuu wa Mali, Moussa Mara, alikua zirani katika mji wa Kidal
kilomita 1,500 kaskazini mashariki na mji wa Bamako.
Katika makabiliano hayo watu 36 waliuawa wakiwemo wanajeshi wanane, na
wengine zaidi ya 30 walitekwa nyara, kulingana na taarifa iliyotolewa na
waziri wa ulinzi Soumeylou Boubeye Maïga.
Kundi la waasi la MNLA limekiri kwamba zaidi ya wanaheshi kumi wa Mali
na wafungwa thelathini waliuawa, na wafungwa wengine wawili
walijeruhiwa, na baadaae walikabidhiwa shirika la msalaba mwekundu.
Hapo jana ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Mali Minusma ilifahamisha
kwamba raia wawili wa kawaida na maafisa sita wa serikali waliuawa
katika mji wa Kidal, bila hata hivo kutoa taarifa zaidi.
Comments