Lilongwe, Malawi. Mahakama Kuu ya Malawi imepinga uamuzi wa Rais wa nchi hiyo, Joyce Banda kufuta matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) kwa madai kuwa hana mamlaka hayo. Mahakama Kuu ilitoa uamuzi huo jana baada ya Rais Banda kufuta uchaguzi huo kwa madai kuwa ulikuwa na kasoro, ikiwa ni pamoja na vitendo vya wizi na matokeo kuchezewa kwenye kompyuta. (Martha Magessa) Wakati Rais Banda akitangaza kufuta matokeo ya uchaguzi alisema: "Ninabatilisha matokeo ya uchaguzi kwa mamlaka niliyopewa na katiba ya Malawi. Ninataka kuwapa Wamalawi nafasi nyingine ya kuchangua mgombea anayefaa kwa uhuru." Aidha, Rais Banda alisema kuwa hatagombea tena nafasi ya urais katika uchaguzi ambao alisema utafanyika ndani ya siku 90 kuanzia sasa. Awali mawakili wa serikali ya Malawi, Kalekeni Kaphale, Noel Chalamanda, Patrick Mpaka waliwasilisha pingamizi mahakamani wakipi...