Skip to main content

Mhe. Lazaro Nyalandu Afanya Ziara Sirari Mara na Kubaini Njia Za Panya

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw John Henjewele(Mwenye suti kulia) akimpa maelezo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu kuhusu eneo linalotarajiwa kujengwa soko kubwa la kisasa katika mji wa Sirari Mkoani Mara.

Kikosi kazi cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara walioongozana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu kutembelea kituo na Masoko ya mpakani katika Mji wa Sirari Mkoani Mara.Mwenye suti katikakati ni Kamanda Joooooooojiiiiiii Maratooooo, wa Aiiiiiii Tiiiiiii Viiiiiiiiiiiiiii.
--

Na Nicodemus Thomas Mushi Info & Comm Officer Ministry of Industry & Trade

Kuimarika kwa ulinzi na usalama katika mpaka wa Tanzania na Kenya katika mji wa Sirari mkoani Mara kumetajwa kuwa chanzo cha kuimarika kwa shughuli za biashara katika eneo hilo.

Hata hivyo, uwepo wa njia nyingi zisizo rasmi na upungufu wa watumishi wa mamlaka za serikali na vitendea kazi katika mpaka huo, umeendelea kuwa sababu inayokwamisha mpango wa serikali wa kukomesha vitendo vya ukwepaji kodi na biashara za magendo katika eneo hilo.

Hayo ni baadhi ya mambo yaliyojiri katika ziara ya ghafla ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, alipotembelea mji wa Sirari katika mwendelezo wa ziara zake za kukagua maeneo ya mipaka ya Tanzania na nchi jirani kwa lengo la kukagua vituo vya pamoja na masoko ya mipakani.

Akimkaribisha Naibu Waziri katika Makao makuu ya Wilaya ya Tarime, Mkuu wa Wilaya Bw John Henjewele na Mbunge wa Tarime Mh Nyambari Nyangwine wamesema, jitihada za serikali za kuimarisha amani na utulivu katika Wilaya hiyo na Mkoa wa Mara kwa ujumla, zimeufanya Mkoa huo kuanza kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa.
“ Tunaendelea kupambana na vitendo vya uhalifu kama biashara za magendo, raia kumiliki silaha kinyume cha sheria, ujambazi na uhasama wa koo za wenyeji wa eneo hili, hali hii ina mchango mkubwa katika kufanikisha shughuli za biashara hasa katika mpaka wetu wa Sirari ambao ukitumika vyema, waweweza kutoa mchango mkubwa kwa pato la Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hizo, Mh Nyalandu amewataka wakazi wa mji huo kushiriki kikamilifu katika biashara halali na kufuata sheria ili kufaidika na fursa zilizopo katika maeneo ya mipakani. Aidha amewataka watendaji wa serikali katika mji wa Sirari kuwasaidia wafanyabiashara wadogo ili washindane na majirani zetu kwa kufika kila wanakofika na kupeleka bidhaa zenye ubora.

Kuhusu agizo la serikali la kupiga marufuku biashara ya sukari kuvuka mipaka ya nchi, Mh Nyalandu amesema... “ Serikali imepiga marufuku biashara ya sukari kutoka nje ya mipaka yetu, sukari inayopatikana nchini ni kwa ajili ya Watanzania, imesamehewa kodi, ni marufuku kuuza nje ya nchi.”

Amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana na wananchi kudhibiti aina yoyote ya magendo katika mpaka huo na kuagiza taratibu za kisheria kuchukuliwa dhidi ya yoyote atakayekiuka kwa makusudi agizo hilo.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...