Kalunde Jamal
KIPA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, na Simba, Juma Kaseja amesema kuwa hana wa kumlaumu kutokana kufungwa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Morocco.Kaseja alisimama langoni katika mchezo ambao Stars ililala mabao 3-1 dhidi ya Morocco katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Afrika 2012. Stars imeaga huku Morocco ikifuzu kutoka Kundi hilo la D.Kaseja alisema kuwa siku zote hapendi kumlaumu mchezaji yeyote kwa kosa ambalo hata yeye angeshindwa kulizuia.Alisema Morocco walijipanga kwa ajili ya ushindi na hata tulipoingia kwenye mji wao, tuliona kweli wamejipanga kufuzu kushiriki fainali hizo."Kwa kweli walituzidi ufundi hakuna wa kumlaumu wala kujilaumu kilichokuwepo tujipange na tuige mazuri tuliyoyaona kwa wenzetu ikiwemo uzalendo uliopitiliza," alisema Kaseja.Alifafanua kuwa pamoja na maandalizi waliyofanya lakini Morocco walijiandaa sana hivyo kama itatokea nafasi ya kushiriki michezo ya kimataifa maandalizi ya kufuzu yafanyike mapema na sio kwenye mechi za mwisho."Kama tunataka kutafuta kufuzu kwenye mashindano yeyote ni vema tukafanya maandalizi mechi za mwanzo kwa kuwa za mwisho kila timu inakuwa imejipanga zaidi ya nyingine kwa kujua ikipoteza nafasi hiyo haitajirudia tena"alisema Kaseja .
Chanzo ni gazeti la Mwananchi.
Comments