Skip to main content

CCM kimepoteza fursa maridhawa Igunga

Tafakuri Jadidi

Johnson Mbwambo
28 Sep 2011
Toleo na 205
“CHAMA Cha Mapinduzi hakikuathirika na mageuzi ya kisiasa na kiuchumi yaliyozikumba nchi nyingine za Afrika. Kinatumia nafasi yake ya kuwa kwenye madaraka kupanga mikakati ya kuendelea kutawala. Mikakati hiyo imekiweka Chama Cha Mapinduzi katika mikono ya wenye madaraka ndani ya serikali ya dola.”
Hayo si maneno yangu; bali ni ya mwandishi wa zamani wa makala za uchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini, ambaye sasa ni mmoja wa washauri wakubwa wa CCM, Prince Bagenda. Maneno hayo yamo katika makala yake kwenye gazeti la Rai, toleo la Oktoba 24-30, 2002 yenye kichwa kinachosomeka; “Chama Cha Mapinduzi bado chama dola”.
“Kinatumia nafasi yake ya kuwa kwenye madaraka kupanga mikakati ya kuendelea kutawala; ndivyo alivyoandika Bagenda katika makala hiyo ya mwaka 2002. Wakati Bagenda akiandika makala hiyo, CCM tayari kilishaanza kupoteza mvuto wake kwa wananchi.
Na kwa hakika, sote tunajua kwamba ni kwa sababu tu ya kuwa chama-dola kiliweza kushinda chaguzi za mwaka 2005 na 2010; vinginevyo kingekuwa tayari kimeishia vilikoishia KANU cha Kenya, UNIP cha Zambia nk.
Naweza pia kuwa na ujasiri wa kusema kwamba kama CCM kitashinda uchaguzi mdogo wa Jumapili ijayo huko Igunga, si kwa sababu kinaendelea kukubalika kwa wananchi; bali ni kwa sababu tu ni chama-dola; hali inayokifanya kiwe katika nafasi nzuri ya kupanga mikakati ya kuchakachua matokeo (DC wa Igunga, Fatuma Kimaro ni ushahidi wa hili).
Nionavyo, uchakachuaji matokeo imebaki kuwa ndio mbinu ya mwisho ya kukibakisha madarakani chama hiki tawala; lakini sote tunajua kwamba mbinu hii si endelevu.
Na kwa mambo yanavyokwenda ndani ya chama hicho na ndani ya serikali yake, hata mbinu hii ya mwisho ya uchakachuaji matokeo haitakisaidia tena chama hicho uchaguzi wa 2015; kwani gadhabu za wananchi dhidi yake zinavyoongezeka ndivyo pia mipango ya kuidhibiti mbinu hiyo inavyoimarishwa.
Gadhabu hii ya Watanzania dhidi ya CCM iliwakilishwa na vijana wale wa Igunga walioamua kuweka staha pembeni na ‘kumshughulikia’ DC yule waliyembamba akiweka mikakati isiyokubalika ya kuhakikisha CCM kinatwaa tena jimbo hilo.
Vijana wale wa Igunga waliopigwa picha wakimburuza mama yule si kwamba walikuwa hawamstahi, na si kwamba walikuwa hawauoni umri wake mkubwa wa kuwa sawa na mama zao; la hasha. Walikuwa wakiyaona na kuyatambua hayo yote; lakini walikuwa wanaongozwa zaidi na gadhabu zao dhidi ya CCM kuliko hekima.
Kwao, DC Fatuma anawakilisha chama kiovu (CCM) kinachopanga kucheza faulo kwenye uchaguzi wao, na hilo pekee lilipandisha hasira zao na kuwafanya watende yale waliyoyatenda ambayo katika hali ya kawaida wasingeyatenda.
Ndugu zangu, inapofikia gadhabu dhidi ya CCM zinawafanya vijana wasiuone na kuuheshimu tena wadhifa wa DC wao; achilia mbali umri mkubwa na jinsia ya anayekishikilia cheo hicho, ujue kwamba siku za mwisho za chama hiki zimekaribia, na kwamba hata hii mbinu ya mwisho iliyobakinayo ya kuchakachua matokeo, haitakiwezesha tena chama hicho kuendelea kukamata dola.
Kwa mtu yeyote makini anayefuatilia mikutano ya hadhara ya CHADEMA mijini na vijijini na kujionea inavyovutia watu, na kwa mtu yeyote anayefuatilia majadiliano ya vijana kwenye mitandao mbalimbali kuhusu hali ya siasa nchini, atakubaliana nami kwamba CHADEMA sasa ni moto wa nyika ambao kuuzima ni shughuli kubwa.
Lakini CHADEMA hakikuibuka tu na kupata umaarufu huu ghafla. Kiliujenga umaarufu wake kidogo kidogo kwa kuyatumia makosa ya CCM ya kutosoma maandiko ukutani na kujirekebisha.
Wanaokumbuka watakubaliana nami kwamba kama CCM kingekuwa sikivu, kingekuwa kimesikiliza tahadhari mbalimbali za mwasisi wake, Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, alizozitoa kati ya mwaka 1987 hadi Oktoba 1999 mauti yalipomfika, na kujirekebisha.
Lakini sivyo kilivyofanya. Kiliweka pamba masikioni na kumkejeli Baba wa Taifa kwamba amepitwa na wakati, na sasa imedhihirika kwamba kumbe chenyewe ndicho kilichopitwa na wakati.
Sasa kinashinda chaguzi zake si kwa sababu ya kuwa na sera makini zinazotekelezeka na zinazowajali wanyonge au kuwa na viongozi makini, jasiri na waadilifu; bali kinashinda chaguzi kwa ujanjaujanja wa kuchakachua matokeo – silaha yake ya mwisho ambayo nayo inakaribia kudondoka!
CCM wakubali au wasikubali; kuna mambo mengi yanayowafanya mamilioni ya Watanzania; hususan vijana, kukichukua lakini kubwa ni suala la ufisadi katika sura zake zote. Hata tafiti zake chenyewe zinaonyesha hivyo – kwamba kinachukiwa kwa sababu ya kukumbatia ufisadi na mafisadi.
Kwa hiyo, katika hali ya kawaida, kama chama hiki kingekuwa na dhamira ya kweli ya kurejesha mvuto wake wa zamani kwa Watanzania, kingelivalia njuga kikweli kweli suala la vita dhidi ya ufisadi. Kwa maneno mengine, kisingekubali kuwa na suluhu na mafisadi.
Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba kimeamua kudhalilisha uwezo wa kufikiri wa Watanzania, kwa kuamua kucheza “usanii” katika jambo nyeti kama hilo linalokera mamilioni ya Watanzania.
Haya majigambo ya ‘kujivua gamba’, kwa mfano, ni mwendelezo tu wa “usanii” ambao kilishaanza kuucheza muda mrefu katika suala la vita hiyo dhidi ya ufisadi na dhidi ya mafisadi.
Hebu fikiria (kwa mfano): Kama kweli CCM kingekuwa na nia ya dhati ya kupambana na ufisadi, si kingelitumia kampeni za Igunga kama uwanja wa kuudhibitishia umma wa Watanzania kwamba sasa kimeamua kikweli kweli kupambana na ufisadi? Kwamba sasa kimeamua kikweli kweli ‘kujivua gamba’!
Lakini kilivyofanya na kinavyofanya kwenye kampeni zake huko Igunga ni tofauti kabisa. Pamoja na ukweli kwamba jimbo hilo limekuwa wazi baada ya mmoja wa viongozi wake, Rostam Aziz, kuamua kujiuzulu kwa kuandamwa na kashfa za ufisadi, CCM kimewakataza wapiga kampeni wake kuzungumzia suala la vita dhidi ya ufisadi wakiwa Igunga, na ikibidi wasitamke kabisa neno “ufisadi” wakiwa kwenye jukwaa la kampeni!
Hatua hii ni ya ajabu kwa chama ambacho miezi michache tu iliyopita kilitaka kuwaaminisha Watanzania kwamba sasa kimeamua kikweli kweli “kujivua gamba” na kupambana na mafisadi mbele kwa mbele.
Kwa hiyo, wananchi wa Igunga wanakwenda katika mikutano yake ya kampeni wakitaraji wapiga kampeni wa CCM kuzungumza kuhusu kero yao kuu na kero ya nchi nzima – ufisadi, lakini hawasikii kauli zozote kuhusu hilo kutoka kwa CCM yao. Kisa? Wapiga kampeni wao wamefungwa mdomo wasitamke neno “ufisadi”, na kwa hiyo, kauli za aina hiyo wana Igunga huzisikia tu kutoka kwa viongozi wa CHADEMA.
Hata pale wana Igunga walipopata ujasiri wa kuwatwanga maswali viongozi wa CCM, mkutanoni, kuhusu ufisadi au hata kuhusu Rostam Aziz, badala ya kuelemishwa ; walifokewa na kununiwa! (rejea kauli ya Wassira huko Igunga ya “Sikuja hapa kuzungumzia ya Rostam”).
Lakini si hilo tu. Kama kweli CCM kingekuwa na nia ya dhati ya kupambana na ufisadi, ambayo ndio kero kuu nchini, kingekuwa kimewapeleka Igunga majemedari wake wanaokubalika kote nchini kuwa mstari wa mbele kukemea ufisadi. Namaanisha watu kama Samwel Sitta, Nnape Nauye, Harrison Mwakyembe, Frederick Sumaye, John Malecela nk.
Mwangwi wa majemedari hao kutoka Igunga kuhusu vita dhidi ya ufisadi na mafisadi ungesikika nchi nzima, na pengine ungesaidia kuwaaminisha baadhi ya Watanzania kwamba kweli, safari hii, kimeamua “kujivua gamba.”
Lakini sivyo kilivyofanya.Watu hawa ambao kingeweza kuwatumia vyema huko Igunga kuithibitishia Tanzania nzima kwamba kweli kimepania ‘kujivua gamba’ na kupambana na ufisadi, wamepigwa marufuku wasikanyage huko Igunga wakati wa kampeni!
Kwa maneno mengine, CCM kimepoteza fursa maridhawa kiliyokuwanayo huko Igunga ya kuwaaminsha Watanzania kwamba kimeamua kikweli kweli kubadilika.
Ni jambo lisiloingia akilini, kwa mfano, kwamba Katibu Mwenezi wa CCM, Nnape Nnauye, anapigwa marufuku asikanyage Igunga katika kipindi cha kampeni. Kwa wadhifa wake ndani ya chama, ni nani tena wanaowajibika moja kwa moja kwenda Igunga kukifanyia chama hicho kampeni na propaganda? Ni kina Rage?
Vyovyote vile; hili ni jambo jingine linalodhihirisha kwamba kweli chama hiki sasa kimeishiwa na waona mbali. Maana; haiingii akilini viongozi wachache ambao CCM bado inao wanaokubalika kwa wananchi (kama Nape) wapigwe marufuku kwenda Igunga kukikampenia chama, na badala yake wapelekwe watu ‘wepesi’ kama Aden Rage ambaye haelewi hata athari za kupanda jukwaani na bastola inayoning’inia waziwazi kiunoni kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi!
Na majemedari hao wa CCM wa vita dhidi ya ufisadi wamepigwa marufuku kwenda Igunga kwa manufaa na matakwa ya nani? Bila shaka ni kwa manufaa ya hao wanaotuhumiwa kwa ufisadi ndani ya chama chenyewe na ndani ya serikali.
Ni dhahiri kama chama hiki kingekuwa na viongozi waona mbali (visionary), kisingefanya hivyo; bali kingeutumia uchaguzi mdogo wa Igunga na majemedari hao kurejesha imani yake kwa Watanzania.
Kingeutumia uchaguzi huo kuwaeleza Watanzania kote walipo ukweli kuhusu dhana yake hiyo ya ‘kujivua gamba’ na vita dhidi ya ufisadi; potelea mbali hata kama ukweli huo ungekifanya chama hicho kipoteze jimbo hilo.
Ni heri kupoteza jimbo moja kwa kuwaeleza Watanzania kote walipo ukweli ili warejeshe imani zao kwa chama hicho, na hivyo kukiwezesha kishinde tena uchaguzi mkuu wa 2015, kuliko kupoteza majimbo yote kwa kucheza “usanii” na kwa kuwahubiria wananchi uongo.
Ndugu zangu, nihitimishe kwa kusema kwamba, kwa jinsi mambo ndani ya CCM yanavyokwenda hivi sasa, twazishuhudia siku za mwisho mwisho za chama hiki kukamata dola.
Siku zaja (na si mbali) ambapo Rais kutoka chama tawala CCM atalazimika kusimama kiungwana jukwaani siku ya kumtawaza rais mpya wa Tanzania na kuyatamka maneno yale machungu ambayo Rupiah Banda wa Zambia aliyatamka wiki iliyopita: “The people of Zambia have spoken and we must all listen”; yaani Wazambia wamechagua, sisi sote hatuna budi kuheshimu waliyemchagua.”
Siku zaja, na haziko mbali; rais kutoka chama tawala CCM naye atasimama na kuitangazia dunia nzima: The people of Tanzania have spoken, and we must all listen”. Siku zaja, na hazipo mbali…!Tafakari.
ambapo Rais huyo mpya atatoka chama kingine na si CCM…! Tafakari.Chanzo ni gazeti la Raia Mwema.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...