Godfrey Dilunga 5 Oct 2011 Toleo na 206 Imedhihirika ni jimbo lililo duni kimaendeleo Hakufanya lolote kubwa kipindi cha ubunge wake KWA takriban miaka mitano, kati ya Oktoba 26, mwaka 1951 hadi Aprili 7, mwaka 1955, Uingereza ilikuwa na Waziri Mkuu aliyeitwa Sir Winston Churchill. Mbali na sifa nyingine za uongozi, alikuwa mpigania ukweli.Katika harakati za kupigania au kutetea ukweli, Sir Winston siku moja alisema: “The truth is incontrovertible. Malice may attack it, ignorance may deride it, but in the end, there it is. Kwamba ingawa ukweli siku zote unaweza kukabiliwa na changamoto nyingi, zikiwamo za uongo, lakini hatimaye hufichuka.Hiki ndicho kilichotokea katika Jimbo la Igunga ambako uchaguzi mdogo wa ubunge umefanyika Oktoba 2, mwaka 2011, kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Rostam Azizi.Rostam amekuwa mbunge wa Igunga kwa takriban miaka 18,kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM). Alichaguliwa kuongoza jimbo hilo kwa miaka mingine mitano katika Uchaguzi ...