Skip to main content

TAMKO KUHUSU KATIBA MPYA YA TANZANIA

TANZANIA GENDER NETWORKING PROGRAMME (TGNP)
P.O. Box 8921, Dar es Salaam, TANZANIA; Gender Resource Centre, Mabibo Road, Adjacent to the National Institute of Transport (NIT) Tel. 255 22 244.3450/ 244.3205/ 244.3286; Mobile 255 7 0754 784050/ 0754 788706; Fax 255 22 244.3244; Email tgnp@tgnp.co.tz; Website www.tgnp.co.tz


Aprili 18, 2011
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba uandikwe upya
Mtandao wa Jinsia Tanzania tumeupokea uamuzi wa Bunge wa kusogeza mbele muda wa kuujadili muswada wa sheria ya mapitio ya Katiba wa 2011 kwa masikitiko makubwa.Uamuzi wa Bunge unaoitaka serikali kuufanyia marekebisho muswada huo na kuutafsiri kwa Kiswahili ni wamsingi ingawa una mapungufu. Tulitarajia kwamba Bunge lingeishauri waziwazi serikali kuuondoa muswada huo Bungeni na kuanzisha mchakato shirikishi wa kutunga muswada mpya.
Kwa hiyo, tunaunga mkono msimamo wa wananchi wanaoitaka serikali kuandaa muswada mpya unaozingatia maoni ya makundi mbalimbali ya wananchi.

Tunapenda kusisistiza msimamo wetu kwamba wananchi hawapaswi kutungiwa sheria ya kuanzisha mchakato na mfumo wa kutunga katiba mpya na chombo chochote kabla hawajajadiliana na kukubaliana juu ya dira, tunu na maadili ya Taifa lao. Msingi wa madai yetu ni mapungufu makubwa yaliyomo kwenye muswada wa marejeo ya katiba wa 2011 uliowasilishwa na serikali Bungeni kwa hati ya dharura. Muswada huu ulitungwa na serikali kabla ya kuanzishwa kwa mjadala wa kitaifa na ndio maana ulikuwa na kasoro nyingi zisizokubalika na watu wengi waliopata wafursa ya kuusoma na kutoa maoni yao.

Tunasisitiza kwamba, mjadala wa kujenga muafaka wa kitaifa unapaswa kuutangulia mchakato wa kisheria wa kutunga katiba mpya. Mjadala wa Kitaifa ndio utakaoainisha: wigo wa uwakilishi wa makundi mbalimbali; sifa za wajumbe wa mkutano wa kitaifa wa katiba na kazi zake; sifa za wajumbe wa tume huru ya katiba na hadidu za rejea za tume hiyo; sifa za wajumbe wa Bunge la Katiba, muundo na kazi zake; na utaratibu wa kuandaa na kusimamia kura ya maoni.
Ili mjadala huo uwe na tija, wananchi wanahitaji muda wa kutosha wa kujadiliana na kukubaliana kwanza juu ya dira, misingi ya kisiasa na kiuchumi na maadili ya taifa lao. Vilevile serikali inahitaji muda wa kutosha wa kukusanya maoni ya wananchi na kuyachambua kabla ya kuandaa sheria ya kusimamia mchakato wa kutunga katiba mpya. Kazi ya kuandaa na kuratibu mjadala wa kitaifa inapaswa kufanywa na chombo huru kinachoundwa na wataalamu wenye misimamo thabiti na sio vyombo au taasisi za dola. Tunaitaka Serikali kuheshimu maamuzi ya wananchi yatakayotolewa wakati wa mjadala huo. Tunasisitiza kwamba maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayozaa sheria nzuri ya mchakato na mfumo wa kutunga katiba mpya.
Tunalitaka Bunge kutimiza wajibu wake wakikatiba kwa kuishauri Serikali juu ya namna bora ya kuandaa na kuratibu mjadala wa kitaifa ili wananchi wote waweze kushiriki kwa amani,utulivu na kuvumiliana. Bunge linapaswa pia kushirikiana na serikali katika kuweka mazingira muafaka ya kisiasa na kisheria ili mchakato wa kutunga katiba ukamilike kwa mujibu wa matarajio ya watanzania wote. Tunawataka wanasiasa wote kutambua wajibu wao wa kutetea maslahi ya taifa na kuepuke kuweka mbele maslahi ya vyama vyao wanapowasilisha hoja zao ndani na nje ya Bunge. Ili kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia haki na wajibu wao wa kuunda katiba mpya, mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa na wadau wote wa siasa nchini:
a) Kuafikiana juu ya mfumo wa kuratibu mjadala wa kitaifa utakaoweka misingi ya kisiasa na kisheria ya kutunga katiba mpya.
b) Kuafikiana juu ya sheria ya kuunda Bunge la katiba na sheria ya kuandaa na kusimamia kura ya maoni. Sheria hizi zitatungwa na Bunge kwa kuzingatia mapendekezo ya wananchi yatakayotokana na mjadala ya kitaifa ulioratibiwa na tume huru ya katiba.
c) Kushirikiana kuweka mazingira muafaka ya kisiasa yatakayowezesha wananchi wote kushiriki katika mchakato wa kutunga katiba mpya bila hofu au kuburuzwa na kundi la watu au taasisi yoyote.
d) Bunge kutotunga sheria yoyote yenye lengo au mwelekeo wa kuchakachua mchakato wa kutunga katiba mpya katika kipindi chote cha mchakato wa kutunga katiba mpya.
e) Kuafikiana juu ya muda wa mchakato wa kutunga katiba.
f) Kuafikiana juu ya namna ya kutoa elimu kwa wananchi wote ili waweze kushiriki ipasavyo katika mchakato wa kutunga katiba.
MJADALA KWANZA, SHERIA BAADAYE!
Imetolewa Dar es salaam na
Mary Rusimbi

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...