Skip to main content

KUMBUKUMBU YA KIFO CHA SOKONE



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Watanzania wana mengi ya kujifunza kutoka aliyekuwa Waziri Mkuu wa tatu wa Tanzania, hayati Edward Moringe Sokoine kwa jinsi alivyokuwa kielelezo cha utumishi wa watu na kielelezo cha kupigania wanyonge.Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumanne, Aprili 12, 2011) wakati akitoa salamu za Serikali katika ibada ya kumbukumbu ya miaka 27 ya kifo cha hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mt. Paulo wa Msalaba mjini Dodoma.
“Marehemu Sokoine atakumbukwa kwa mengi ambayo kwa kweli tukiyaongelea hapa hatutayamaliza; ninachoweza kusema, leo tunamkumbuka mtu ambaye kwetu sisi Watanzania, ni kielelezo bora cha utumishi wa watu, kielelezo cha kujituma, kielelezo cha upendo, kielelelzo cha kupenda haki kielelezo cha kupigania wanyonge na kielelezo cha kumcha na kumtumikia Mungu,” alisema.

Alisema katika utumishi wake, Mzee Sokoine alifanya bidii kutetea wanyonge na maslahi yao kwa kupambana na watu wanaohodhi bidhaa (walanguzi na wahujumu uchumi) hadi wakasalimu amri. “Wakati akitangaza vita dhidi ya walanguzi, nakumbuka alitoa kauli hii: Kama wanasema Serikali ilikuwa likizo, sasa wajue kuwa likizo imekwisha,” alisema Waziri Mkuu akimnukuu hayati Sokoine.“Alitumia muda mwingi kujenga jamii inayochukia rushwa na ulanguzi... Japo hayupo kati yetu kimwili, faraja ninayoipata mimi kama Pinda, tunapoadhimisha kumbukumbu kama hii ni kuwa bado huyu mwenzetu tuko naye kimawazo, kiakili na kubwa zaidi kiroho,” alisema.

Mkuu alisema marehemu Sokoine alikuwa kiongozi wa kipekee kwani aliamini kwamba, kuwajibika kama kiongozi ni kukubali kwa hiari dhamana ya uongozi unayopewa ama kwa njia ya kuomba kwa kura au kwa kuteuliwa Kikatiba au Kisheria. “Aliamini kuwa Kiongozi lazima akubali kutumia dhamana ya uongozi aliopewa kwa maslahi ya umma na kwa Taifa kwa ujumla.”

Waziri Mkuu Pinda alisema: “Marehemu Sokoine amefanya mengi mazuri ambayo tunayakumbuka leo. Hebu tujifunze kutoka kwake kwamba; mazuri tunayoyafanya leo, huwa furaha ya kesho. Tumuige kwa kufanya mazuri ambayo yatakumbukwa daima na vizazi vijavyo,” alisema.
“Marehemu Sokoine alikuwa muasisi wa biashara huria nchini wakati tukiwa kwenye itikadi ya Ujamaa. Aidha, alikuwa na wazo zuri la kuanzisha usafiri wa daladala Dar es Salaam. Wakati wake mabasi makubwa ya ofisini yalitumika kubeba watu Jijini Dar es Salaam na hii ni kielelezo cha kuujali umma wa Watanzania,” alisema.

Mapema akitoa mahubiri katika ibada hiyo, Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Askofu Gervas John Nyaisonga alisema kumbukumbu ya kifo cha Sokoine iwakumbushe Watanzania ni nini cha kujifunza kutoka kwake kuenzi tunu alizoacha.
Alisema alikuwa mtu wa kipekee kwani alijitolea kukatwa asilimia 50 ya mshahara wake ili kuchangia katika mfuko wa nguvukazi ili wananchi wasio na uwezo wa kukopa benki waweze kupata mikopo kutoka katika mfuko huo.

Ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Nyaisonga kwa kushirikiana na mapadri wengine saba ilihudhuriwa na wanafamilia wa Sokoine, Spika wa Bunge, Bibi Anna Makinda, Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Edward Lowassa, Wabunge, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wakuu wa wilaya na waumini mbalimbali kutoka Dodoma, Mvomero na Arusha.
Edward Moringe Sokine ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 46, aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa vipindi viwili cha kwanza kikiwa ni Februari 13, 1977 hadi Novemba 7, 1980 na kipindi cha pili kuanzia Februari 23, 1983 hadi Aprili 12, 1984 alipofariki kwa ajali ya gari Wami Dakawa, mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam kutoka Dodoma ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa Bunge.
IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI MKUU,S. L. P. 980,DODOMA.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was

HAYA NI MAKAO MAKUU YA MTANDAO WA Tigo TANZANIA DAR ES SALAAM

MAHALA yalipo ni Lugoda Street Gerezani Industrial Area , kwa sasa mdandao huu umefanya makubwa , kuna Tigo Bwerere Uilisha cheki hiyoooooo watu full kujiachia wana chonga tuu kwenye vyao vilonga.