Kwa mara nyingine tena Times radio fm imeandaa Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lenye kauli mbiu isemayo “MITIKISIKO YA PWANI 2010 NI ZAIDI YA BURUDANI”
Mitikisiko ya Pwani - Burudani ya Taarabu ilianzishwa miaka mitatu iliyopita na hadi sasa imeendelea kuvutia wapenzi wengi wa muziki wa Taarabu, na utamaduni wa pwani na hivyo kuwa tukio maarufu hapa Tanzania hususan Dar es salaam.
Mwaka jana Mitikisiko ya Pwani ilifanyika kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba ikiwa na lengo la kuvitambulisha na kuzisaidia bendi bora za muziki wa Taarabu Jijini Dar Es Salaam huku likihudhuriwa na maelfu ya watu.
Burudani ya Mitikisiko ya Pwani mwaka huu ina madhumuni ya kusaidia jamii na pia kutoa burudani kwa wapenzi wa Taarabu na Watanzania kwa ujumla.
Tamasha hili litakuwa nafasi kubwa ya wapenzi wa muziki wa Taarabu kusikiliza, kuangalia na kucheza tungo bora kutoka kwa bendi zote mahili za Taarabu nchini.
Zawadi kadhaa zitatolewa kwenye Tamasha hilo ikiwa pamoja na zawadi kutoka kwa wadhamini wetu, oryx wauzaji wa mafuta, gesi na majiko ya gesi nchini pamoja na fedha taslimu ambazo zitachukuliwa na wapenzi wa Taarabu huku watu mia moja wa kwanza watajipatia t-shirts.
Mpaka sasa ni bendi tisa ambazo zimethibitisha kushiriki katika tamasha hilo ambalo litafanyika 03/12/2010 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee huku likimshirikisha msanii mkongwe wa Taarabu, Bi kitude ambaye pia mbali na kutumbuiza atakabidhiwa Tuzo ya Heshima kulingana na Mchango wake wa muziki kwa muda mrefu.
Bendi hizo ni pamoja na:
1) Coastal Modern Taarab
2) Dar Modern Taarab
3) East African Melody
4) Five Star Modern Taarab
5) Jahazi Modern Taarab
6) New Zanzibar Modern Taarab
7) Super Shine Modern Taarab
8) Tandale Modern Taarab
9) TOT Taarab
Tunawashukuru Mazula,Public Relation officer ,100.5. Times Radio fm
+255713412872
+255787412872
sana wadhamini wetu ambao ni ORYX, wauzaji wa mafuta, gesi na majiko ya gesi nchini, Tigo, Regency Hotel, PSI, ICV Security Company, Malaika Beach Resort, Zizou Fashion, Dida classic boutique, Jolyety Saloon.
Comments