Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi kadi kwa mmoja wa watoto waliojiunga na bima ya afya ya watoto (TotoAfyaCard) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya (NHIF) Spika Mstaafu Mama Anne Makinda na kushoto ni Benarld Konga Kaimu Mkurugenzi wa Mkuu wa (NHIF).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amezindua (TotoAfyaKadi) Bima ya Afya kwa watoto. katika uzinduzi uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam aki, Kwa mujibu wa Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), kati ya Watanzania 52m waliopo sasa (2017) watoto ni 26.7m (sawa na 51%). Mtoto ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18.
Ummy Mwalimu anasema (TotoAfyaKadi) ni njia sahihi ya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote nchini. Mpango huu unatoa Uhakika wa Matibabu kwa mtoto kwa Tshs 50,400/= kugharamia matibabu yake kwa mwaka mzima. Tena sio kwa Vituo vya Serikali bali pia vya Binafsi. Lakini pia si kwa Halmashauri au Mkoa unayoishi bali nchi nzima.
Waziri Ummy Mwalimu ameongeza kusema “Wazazi na Walezi wenzangu Ugonjwa huja bila Taarifa! Tuchangamkie (TotoAfyaKadi) ili kuwa na uhakika wa matibabu ya Mtoto kabla ya kuugua kwani Mwenye Macho haambiwi Tazama. (TotoAfyaKadi) ndio mpango mzima.
Comments