SERIKALI kununua mtambo wa kutibu kansa ya mionzi wenye thamani ya Shilingi
billion 14.5, hayo yamesemwa jana na Naibu waziri wa Afya Dakt Khamis Kigwangala
alipokuwa akifungua mafunzo ya kansa ya mionzi katika Taasis ya Saratani
(Ocean Road Hospital) jijini Dar es Salaam.
Kigwangala amezungumza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kufunguliwa mafunzo hayo ya wiki moja yanayofanyika nchini.
“Kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa saratani nchini kuzidi kuongezeka,serikali katika bajeti yake yamwaka 2017/18 imetenga kiasi hicho cha fedha katika kukabiliana na magonjwa ya kansa.
Mtambo huo wenye uwezo wakugundua kila aina ya kansa ,kwasasa upo Afrika ya
Kusini pekee katika bara la Afrika hivyo endapo Tanzania itanunua mtambo huo
itaokoa maisha ya watu wengi sana.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road Dakt Julius
Mwaiselage amesema miongoni mwa kansa inayongoza Tanzania ni ile saratani
ya mfuko wa uzazi kwa asilimia 40 ikifuatiwa na saratani ya matiti kwa asilimia
kumi.
Hata hivyo amesema ongezeko kubwa la saratani nchini husababishwa na watu
kubadirisha mfumo wa maisha hususani kutokuzingatia mazoezi pamoja na ulaji
usiofaa(mbovu).
Dakt Mwaiselage amesema ,Watanzania walio wengi hawana tabia yakupima afya
mara kwa mara kwani hufikishwa kituoni hapo kansa ikiwa katika kiwango cha
juu sana ambapo uwezekano wakupona unakuwa mdogo sana.
Kwa mujibu wa Dakta Mwaiselage takribani watu elfu arobaini hugundulika kuwa
na ugonjwa wa kansa na kati ya hao watu wapatao 30,000 hufa kwa mwaka hii yote
husababishwa nakutokuwahi tiba ya ugonjwa huo.
Mafunzo hayo yakubadirishana uzoefu katika maswala ya kansa umeweza
kuwakutanisha matabibu mbali mbali kutoka nchi za bara la Afrika ikiwemo,
Siera Leon,Namibia,Tanzania,Kenya,Afrika ya kusini na visiwa vya Comoro,
Shelisheli na Madagasca.
Comments