WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiwa anamsikiliza Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto mara baada ya kuwasili katika banda hilo hivi karibuni jijini Arusha katika maadhimisho ya sikukuu ya nane nane Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa na watanzania. Na Pamela Mollel,Arusha WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama amezitaka hifadhi za taifa nchini kuendelea kuwatumia wasanii nchini katika kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana huku akiipongeza Mamlaka ya hifadhi za taifa Ngorongoro inavyotangaza vivutio vyake kupitia msanii Mrisho Mpoto. Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni jijini Arusha alipotembelea banda la Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro katika maonesho ya Nanenane. Alisema k...