Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akitoa hotuba ya uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa kutathmini maendeleo ya sekta ya maji uliowashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa arnautoglo uliopo maeneo ya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa maendeleo wa sekta ya maji walioshiriki katika Mkutano Mkuu wa kutathmini maendeleo ya sekta hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa arnautoglo uliopo maeneo ya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam. Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Wizara ya Maji na Umwagiliaji imejipanga kuanza ujenzi wa mtambo mkubwa wa majitaka katika maeneo ya Ilala Jijini Dar es Salaam ili kuzuia uchafuzi wa mazingira nchini. Hayo yamesemwa leo ...