Skip to main content

Tamasha La Pasaka Lasaidia Wahanga Wa Gongo La Mboto Laja

Promotions wanadaaji wa Tamasha kubwa la Pasaka , Alex Msama amesema kwamba kiasi cha fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo, zitatumika kuwasaidia waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.



Msama amesema hayo baada ya kuwakabidhi waathirika wa milipoko hiyo msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya ya shilingi mil 3.



Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ndiye aliyekabidhi msaada huo jana katika ofisi ya redio ya Clouds FM iliyoko Mikocheni, Dar es Salaam.



Vitu vilivyotolewa ni magunia manne ya mchele, kila moja likiwa na kilo 120, magunia mawili ya maharage, magunia 10 ya unga wa mahindi, mifuko miwili ya sukari, mifuko mitatu ya unga wa ngano yenye kilo 25 kila moja na ndoo mbili za

mafuta ya kupikia.



Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Msama alisema wameguswa na waathirika hao, na pia wanafanya hivyo ikiwa ni kutimiza moja ya malengo ya tamasha hilo.



Msama alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za milipuko hiyo kwa Watanzania, na ndiyo maana wamejitolea kusaidia waathirika kwa misaada ya vyakula.



“Lengo kubwa la tamasha la Pasaka linaloratibiwa na Msama Promotions ni kusaidia watoto yatima na jamii kwa ujumla... hata hawa wenzetu walioathirika kwa kwa mabomu hatuna budi kuawasaidia.



"Natoa mwito kwa Watanzania wenzangu kuwa na moyo wa huruma na kuwasaidia waathirika hawa wa mabomu na pia naishukuru Clouds FM kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha Watanzania kutoa misaada," alisema Msama.

Akipokea msaada huo, mtangazaji wa Clouds FM, Anthonio Nugazi anayeendesha kipindi cha Kambi Popote, alimshukuru Msama kwa kuonesha moyo wa kujitolea, na akatoa mwito kwa Watanzania wengine kuiga mfano.

Nugazi alisema Clouds 88.4 FM watawasilisha michango hiyo kwa wahusika katika kambi waliyoianzisha ya kutoa msaada Shule ya Msingi Mzambarauni iliyopo Ukonga, Mombasa, Dar es Salaam.

Tamasha la Pasaka la nyimbo za Injili za kumsifu Mungu, litafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Apili 24 mwaka huu na litashirikisha wasanii kutoka nchi sita za Afrika wakiwamo waimbiaji kutoka Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Lengo la tamasha la mwaka huu ni kupata fedha zitakazotumika kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wajane.

Milipuko hiyo iliyotokea katika kambi ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha 511 KJ, iliyopo Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ilisababisha vifo vya watu 20 huku wengine zaidi ya 300 wakijeruhiwa.

Pia milipuko hiyo ilisababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi huku wengi wakipata hifadhi kwenye Uwanja wa Uhuru wakiwamo watoto wadogo waliopotezana na wazazi wao.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Mwana muziki Marufu kwa jina la Chuck Brown Afariki Dunia Akiwa na umri wa miaka 75

View Photo Gallery — Chuck Brown dies at 75: The “godfather of go-go” has died By Chris Richards, Updated: Wednesday, May 16, 4:42 PM Chuck Brown, the gravelly voiced bandleader who capitalized on funk’s percussive pulse to create go-go, the genre of music that has soundtracked life in black Washington for more than three decades, died May 16 at the Johns Hopkins University hospital in Baltimore. He was 75. The death, from complications from sepsis, was confirmed by his manager, Tom Goldfogle. Mr. Brown had been hospitalized for pneumonia. Known as the “Godfather of Go-Go,” the performer, singer, guitarist and songwriter developed his commanding brand of funk in the mid-1970s to compete with the dominance of disco. Like a DJ blending records, Mr. Brown used nonstop percussion to stitch songs together and keep the crowd on the dance floor, resulting in marathon performances that went deep into the night. Mr. Brown said the style got its name because “the music j...