BAADA ya kuzindua albamu aliyoipa bila ya kumshirikisha msanii yoyote, mwimbaji nyota wa kundi la Tanzania House of Talent (THT), Elias Barnaba amesema kuwa sasa anataka kuwashirikisha wasanii wa Afrika Mashariki katika albamu yake ya pili.Barnaba alikuwa ni miongoni mwa wasanii wa THT wakati wa hafla ya kuazimisha miaka mitano ya kundi hilo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Wakati msanii huyo mwenye sauti tamu akizindua albamu yake ya Kichwa Changu', wasanii wengine waliozindua albamu zao katika hafla hiyo ni Doto Kalengeza 'Dito', Amini Mwinyimkuu, Mwasiti Almasi na Linah.Albamu ya 'Kichwa Changu' imebeba nyimbo za Sipendi Dharau, Samahani, Tulizana,na Some Day kilichopigwa na mwanamuziki Lokua Kanza kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo [DRC]Barnaba alisema kuwa ameamua kuwashirikisha wasanii wa Afrika Mashariki ili kuongeza utamu zaidi ndani ya nyimbo zake."Albamu ya kwanza nilikuwa nataka kuonyesha uwezo wangu, lakini katika albamu yangu ya pili nataka kuonyesha uwezo wangu katika kushirikiana na wasanii wenzangu wa aina mbalimbali," alisema Bartnaba.

Comments