Mbunge
wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akifunga mkutano wa
wadau wa habari mkoa wa Iringa ,mkutano ulioandaliwa na chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Iringa na muungano wa vilabu vya waandishi
wa habari Tanzania (UTPC)
Wabunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao (chadema) kulia na Ritta Kabati wakijadiliana mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa habari leo mjini Iringa
Baadhi ya wanahabari mkoa wa Iringa wakisikiliza maoni ya wadau wa habari
mbunge wa jimbo la Iringa Mchungaji Peter Msigwa(Chadema) akiwa na mbunge wa viti maaalum mkoa wa Iringa Mhe.Chiku Abwao (Chadema) wakisikiliza michango ya wadau wa habari leo
Mkuu wa chuo cha Tumaini Prof.Nicholaus Bangu kulia ,mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wakisikiliza mijadala ya wadau wa habari leo
Viongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) wakiwa na wadau mbali mbali mara baada ya mkutano wao leo
Mtoa mada katika mkutano wa wadau wa habari Iringa Saimon Belege kulia akipongezwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Chiku Abwao nje ya ukumbi wa Manispaa ya Iringa
Wabunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Chiku Abwao (chadema) kulia na Ritta Kabati wakijadiliana mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa habari leo mjini Iringa
Baadhi ya wanahabari mkoa wa Iringa wakisikiliza maoni ya wadau wa habari
mbunge wa jimbo la Iringa Mchungaji Peter Msigwa(Chadema) akiwa na mbunge wa viti maaalum mkoa wa Iringa Mhe.Chiku Abwao (Chadema) wakisikiliza michango ya wadau wa habari leo
Mkuu wa chuo cha Tumaini Prof.Nicholaus Bangu kulia ,mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) wakisikiliza mijadala ya wadau wa habari leo
Viongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) wakiwa na wadau mbali mbali mara baada ya mkutano wao leo
Mtoa mada katika mkutano wa wadau wa habari Iringa Saimon Belege kulia akipongezwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mhe.Chiku Abwao nje ya ukumbi wa Manispaa ya Iringa
MKUU wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa Profesa Nicholaus Bangu ameitaka wizara ya elimu nchini kuangalia uwezekano wa kuboresha zaidi mitaala ya elimu kwa kuongeza somo la usomaji wa magazeti kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuwawezesha vijana wengi zaidi kuipenda taaluma hiyo na kuongeza nguvu zaidi ya usomaji wa magazeti.
Prof.Bangu alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mkutano wa wadau wa habari ulioandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) kwa ufadhili wa muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na kufanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa na wahabari katika kuibua mambo mbali mbali ila bado vyombo vya habari vinapaswa kufanya tathimini na kujua habari zinazoandikwa zinasomwa kwa kiwango gani .
Hivyo alisema kuwa njia pekee ya kuongeza nguvu ya usomaji wa magazeti hapa nchini ni vyombo vya habari kujenga mahusiano zaidi na wizara ya elimu ili kuangalia uwezekano wa kuingiza somo la usomaji wa magazeti katika vipindi mashuleni.
Prof.Bangu alisema kuwa kwa mtazamo wake usomaji wa magazeti nchini umeendelea kushuka zaidi pamoja na kuwepo kwa ongezeko kubwa la magazeti hayo na kuwa iwapo wasomaji wa magazeti itapungua kuna uwezekano wa waandishi wa habari kuendelea kununuliwa na watu wachache wenye pesa ili kuendelea kuwaandikia habari zao.
Hata hivyo alisema kuwa mwenendo wa uandishi wa habari wa magazeti kwa sasa unatia kichefu chefu kutokana na baadhi ya magazeti kila linapotoka kuandika habari za kuishambulia serikali kwa mabaya pekee huku mazuri yakiachwa hali inayopelekea wasomaji kuchukia magazeti hayo .
Katika hatua nyingine Profesa Bangu alitaka vyombo vya habari nchini kubadilika kwa kujikita kuandika habari za uchumi na zile za kijamii kwa ngazi ya chini zaidi badala ya kuendelea kuandika habari za kitaifa pekee.
Alisema kuwa iwapo wanahabari nchini watajikita kuandika habari za uchumi upo uwezekano wa maslahi yao pia kuweza kuboreshwa kutokana na kazi wanayoifanya.
Kwa upande wake Rais wa UTPC Keneth Simbaya aliwataka wanahabari nchini kuweza kubadilika kwa kujikita kuandika habari zenye kulijenga Taifa na sio kulibomoa Taifa.
Alisema kuwa hakuna ubishi kuwa Taifa limeweza kufika hapa tulipo kutokana na kazi nzuri ya vyombo vya habari na kuwa kazi hiyo nzuri inapaswa kuendelea kuenziwa na wanahabari nchini kwa kufanya kazi zenye maadili zaidi.
Pia alitaka wadau wa habari kuendelea kusaidia vilabu vya waandishi wa habari nchini ili kuweza kusonga mbele zaidi.
Akizungumzia mahusiano kati ya waandishi wa habari na viongozi mdau wa habari Mzee David Butinini alisema kuwa bado vyombo vya habari nchini vimeendelea kunyimwa ushirikiano na viongozi wa serikali .
Huku akitaka waandishi wa habari kuendelea kuandika habari za vijijini zaidi badala ya kuandika habari za semina na zile za watu wanaowalipa posho ili kuweza kuziandika habari zao.
Butinini alisema kuwa itapendeza kuona waandishi wa habari wakiandika habari za kilimo zaidi na kuona kuwa sera ya kilimo kwanza inatekelezwa kwa vitendo badala ya ilivyo sasa ambapo kilimo kwanza kimekuwa kikizungumziwa katika vyombo vya habari pekee badala ya kuandika utekelezaji.
"Nawaombeni sana waandishi wa habari kuacha kuogopa katika kuendelea kuwatumikia wananchi katika tasnia ya habari ....kwani iwapo waandishi wa habari watashindwa kutumikia vema wananchi "
Baadhi ya wadau wa habari mkoani Iringa wameeleza malalamiko yao juu ya utendaji kazi wa vyombo vya habari na kuwa vimekuwa haziibui habari za kijamii na badala yake kuegemia habari za mshiko zaidi hasa za wanasiasa ambao wamekuwa wakipenda kupongezwa hata wanapofanya mabaya.
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) alitaka waandishi wa habari mkoani Iringa kubadilika na kutoogopa mtu ama kuandika habari za huruma kwa mwanasiasa asiyetimiza wajibu wake.
Alisema kuwa kazi ya vyombo vya habari ndani ya mkoa wa Iringa na Taifa imeendelea kuzaa matunda zaidi na kuwa umefika wakati wa waandishi kufunguka zaidi kwa kupenda kujisomea vitabu mbali mbali ili kuboresha utendaji wao.
Huku mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati akipongeza vyombo vya habari huku akitaka wadau wa habari kuacha kuzitolea macho posho za wabunge na kusahau idara nyingine za serikali ambazo pia wanalipana posho kubwa tena kwa maslahi yao binafasi.
Alisema kuwa posho za wabunge zimekuwa zikiliwa na wengi hadi ngazi za chini ila wakuu wa idara za serikali wamekuwa wakijilipa posho ambazo mwisho wa siku zinaishia kwao pekee.Na mdau francisgodwin.blogspot.com
Comments