Vigogo wa NASA kuanzia kulia, Isaac Ruto, Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula
Wanawake na vijana nchini humo pia wameahidiwa kupewa nafasi kubwa katika serikali ya NASA na kutobaguliwa.
Pamoja na hilo, vita dhidi ya ukabila, ni mojawpao ya suala ambalo Odinga amesema atalishughulikia kwa kuhakikisha kuwa nafasi ya kazi zinagawanywa kwa usawa ili kuhimiza umoja wa kitaifa.
Baada ya uzinduzi wa ilani ya chama tawala Jubilee na muungano wa NASA, kampeni zinaendelea kama kawaida katika maeneo mengi ya nchi hiyo, kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe nane mwezi Agosti.
Dokta Brian Wanyama, mchambuzi wa siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kibabii nchini Kenya, anasema pamoja na kuzinduliwa kwa Ilani hizo, wananchi wengi huenda wasibalishe mitazamo na maamuzi yao kwa sababu siasa za Kenya zinaegemea ukabila na ukanda.
“Itakuwa vigumu sana kwa Wakenya kubadilisha mitazamo yao kwa sababu za siasa za kikabila,” asema Wanyama.
Comments